Nukuu za maisha

1. Sio yote utakayofunzwa na mwalimu wako darasani .Hapana mengine  utayapata hapa mitaani,ya kujenge na kubomoa moyo wako utayapata ,fitina umbeya chuki na usaliti wa kimapenzi yote yapo kama haujayapata Shukuru MUNGU ni machungu nakwambia

2.  Waliofanikiwa nenda ukawaulize ,wakuambie maumivu na magumu waliyopitia hadi wafike hapo walipo.Ndipo utagundua kwamba dunia haina huruma na wala haina mwenyewe.Maumivu ni sehemu ya maisha na yapo kwa kila mtu.Usichoke endelea kupambana.Ukianguka  inuka endelea na safari MUNGU mbele

3. Brother starehe zipo tu, wanawake wazuri wapo tu, unachokipata kwa jasho lako leo kitunze sana ili ukifanyie mahitaji yako ya muhimu kwa ajili  ya future yako halafu starehe ni wewe na familia yako

4. Hakuna kitu kinaturudisha nyuma kiuchumi sisi wanaume kama MAHUSIANO

5. Ubora wa maisha yako unachangiwa na ubora wa mahusiano yako. Ukiona mahusiano uliyonayo yanakutoa kwenye reli ya maisha basi  nakushauri jitoe mapema kwenye mahusiano hayo

6. Usikubali mapenzi yakutese, usikubali mtu akukoseshe amani na furaha eti kisa unampenda, usikubali kumnyenyekea mtu eti kisa unampenda, usikubali . Ukiona hakuelewi , ukiona anakusumbua, ukiona ana tabia za ajabu MUACHE AENDE usimlazishe mtu akupende wakati yeye hataki   kukupenda.

7. Hicho kidogo ulichonacho ni MBEGU ambayo umekabidhiwa ili ikusaidie Kukua, inawezekana kabisa hakilingani na unachokitaka ila usikidharau. Inawezekana kazi uliyonayo sasa haifanani na kazi unayoitaka, Nikukumbushe jambo moja HAKUNA NYAKATI INAYODUMU KWENYE MAISHA YA  MTU  VUMILIA

8. Ukiona ulikuwa na mtu kwenye mahusiano mda mrefu halafu likatokea tatizo tu kidogo ghalfa akapata ujasiri wa kukwambia TUACHANE basi ujue huyo toka mwanzo alikuwa na mtu or kama hakuwa na mtu basi ujue alikuwa na mpango wa kukuacha kwahiyo acha kuhangaika naye MUACHE aende


9. Usipoteze mda wako kumufikiria mtu aliyekuumiza kwasababu utashindwa kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yako. Jifunze sana kufikiria yaliyopo mbele yako na ya nyuma yaache kama yalivyo, kubali kuwa maumivu ni sehemu ya kufanikiwa na kujifunza


10. Hakuna kitu chenye mwanzo kikakosa mwisho , kila kitu unachokiona  katika dunia hii kina mwanzo wake na mwisho wake pia. Hayo maumivu ya kuachwa unayopitia leo yana mwisho wake, hayo maisha magumu unayopitia leo ipo siku mwisho wake utafika, Usiogope wala usikate tamaa  yatakwisha

11.  Kubali yalitokea , tulia na uache kulia,futa namba yake na umtoe akilini mwako.Usijilazimishe kwa mtu asiyekuhitaji,jifunze kulinda thamani  yako. 

12. Kila mtu ana mapito, Kila mtu hukosea kufanya maamuzi, Hivyo kamwe usikae chini kumjadili mtu ili hali na wewe una mapungufu.

13. Hakikisha ukiwa unatoa ahadi uwe unamaanisha na unatimiza. Ahadi inaweza kukuongezea ama kukupunguzia thamani kwa watu unaowaahidi, Fikiri kabla ya kuahidi

14. Maumivu  yanakuwa makali zaidi ukigundua hata yule aliyekuambia anakupenda hakupendi alikuwa muongo na mwigizaji tu, kwenye maisha  yako.Licha ya haya maumivu yote usiache kuwa na imani na kuamini  MUNGU. Kulikuwa na sababu ya mbona uliyapitia hayo. iwapo    haukujifunza kitu basi yeye,alijifunza kitu toka kwako.

15. Mheshimu na umjali sana huyo uliye naye kisha umpe MUNGU utukufu na ndoa yenu itafanikiwa  usije ukaruhusu  dhambi ikatawala ndani  yako,MUNGU anakataa

16. Kumbuka,kufanikiwa kwenye elimu peke yake hiyo haitoshi .Tupo kwenye dunia ambayo ukiwa na fedha unaheshimika sana kuliko mwenye  masomo na vyeti vyake kando na elimu Hakikisha unapambana sana kufanikiwa kwenye eneo la pesa,

17. Atakayekuvumilia wakati wa shida , Huyo ndo mpenzi wa kuwa naye wakati wa raha. wengine achana nao

18. DUNIA INAZUNGUKA. Usipende kuwafanyia watu vitu usivyo penda kufanyiwa.

19. Uvumilivu ni dalili ya Ushindi,jifunze kuvumilia kwa kila jambo Yaani kuna mtu umempa umuhimu mkubwa maishani mwako, 
      Lakini  wewe hauna maana kwake hata kidogo.Hata ukifa hashituki , jifunze kujipa umuhimu kwanza kabla ya kumpa mwengine.

20. Ukiona kinachomwagika kiache kimwagike,na iwapo kinataka kuvunjika kiache kivunjike, na anayetaka kuondoka muache aondoke .Itambue thamani yako na ujiamini

21. Hakuna mtu yuko vizuri kwa kila jambo,Kila mmoja ana mapungufu yake, kwa hiyo unaposema eti unamwacha mtu kwa sababu ya mapungufu yake, Jiulize kama wewe ni mkamilifu.Tujifunze kuvumiliana

22. Mpenzi wako sio kiumbe dhaifu, Bali ishi naye kama kitu kilicho dhaifu, Umpe uangalifu kama mtu aliyebeba kioo au trei ya mayai, Mtapendana  sana hadi kifo.Niamini

22. Ukitaka kujua tabia ya mwanaume, Tazama jinsi anavyoishi na watoto na Sio watu wa rika lake.

23. Ni wewe pekee unayeweza kubadili maisha yako, Hakuna mwengine anayeweza kukubadilishia.

24. Mafanikio hayaji kama ajali, Bali huja kwa kazi ngumu,Uvumilivu,Kujituma,Kujifunza,Kujitoa na zaidi ya yote Upendo kwa kile unachofanya au kujifunza kufanya

25.Kamwe usikubali kushindwa pasipo kupambana.

25.Usilie kwasababu limeisha, Bali tabasamu kwasababu limetokea

26. Kwa maneno matatu naweza kuelezea kilakitu nilichojifunza kuhusu Maisha, “Yana Kwenda Mbele”

27. Mwishoni, Tutakacho kumbuka si Maneno ya maadui zetu, Bali ni kimya cha marafiki zetu.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *