Kikembe ni udogo wa neno mkembe ambaye ni mtoto mdogo
mwenye umri baina ya mwaka mmoja na sita.
Kuna aina mbalimbali ya wanyama sawa na vikembe vyao.
Ifuatayo ni mifano ya vikembe
Kikembe cha mbwa ni kibwa, kilebu kidue.
Kikembe cha mbweha ni nyamawa.
Kikembe cha sungura ni kitungule, kituju.
Kikembe cha punda ni kilongwe, kihongwe , kipura.
Kikembe cha ndovu ni kidanga.
Kikembe cha ng’ombe ni urusi, ndama.
Kikembe cha kuku ni kifaranga.
Kikembe cha ndege ni kinda.
Kikembe cha nyoka au mtambaachi ni kinyemere.
Kikembe cha chui ni kisui,chongole.
Kikembe cha asadi au simba ni shibli, kibuai.
Kikembe cha fisi ni bakaya, kikuto.
Kikembe cha nyani ni kigunge.
Kikembe cha nyuki ni chana, jana.
Kikembe cha nondo au kipepeo ni kiwavi.
Kikembe cha nzi ni bombwe, buu.
Kikembe cha nzige, ngeda pia cha panzi ni maige,tunutu, funutu,matumatu.
Kikembe cha chura.Pia mbu ni kiluwiluwi.
Kikembe cha papa ni kinengwe.
Kikembe cha samaki ni kichengo
au chengo
Kikembe cha nyangumi ni kinyangunya,chengo.
Kikembe cha mamba/ngwena ni kigwena.
Kikembe cha nge ni kisuse.
Kikembe cha binadamu ni mwana au kinyandu.
Kikembe cha paa ni kipaa.
Kikembe cha meza ni dawati, jarari.
Kikembe cha tai ni kikangazi.
Kikembe cha mdudu ni kingonyo.
Kikembe cha kwanga/wibari ni kitungule.
Mtoto wa jicho ni kingo.
Kikembe cha panya ni kigoso.
Kikembe cha tumbili ni chachuli.
Kikembe
cha kipepeo ni kiwavi.
Mtoto
wa mtumwa ni mjoli
Kikembe cha chungu au sisimizi ni kwida.
Kikembe cha funza ni kongonyo.
Kikembe cha paka ni kinyaunyau,kipusi
Kikembe cha farasi ni kitekli.
Kikembe cha farasi na punda
ni baghala ,nyumbu.
Kikembe cha mbuzi ni kibuli kimeme, kibui,
tangina.
Kikembe cha kondoo au ng’onzi ni katama, kibebe.
Kikembe cha nguruwe ni , kiguruwe,kivininde kivinimbi.
Kikembe cha ngamia au bairi ni nirihi. nirigi