Maamkizi hutumika kujuliana hali.
Ni maneno ya kuamkiana. Kuna maamkizi yanayoweza kutumika nyakati zozote na baina ya watu wowote.
Maamkizi na Majibu
1. Habari? – njema/nzuri
2. Uhali gani? – njema/nzuri
3. Je la utu? – sina utu
4. Waambaje? – sina la kuamba/salama
5. Sabalkheri? – sabalkheri/aheri
6. Masalkheri? – masalkheri/aheri
7. Alamsiki? – alamsiki binuru
8. Shikamoo/ – marahaba / kuzinawe nashikamoo?
9. Chewa? – chewa
10. Salaam aleikum – aleikum salaam
11. Buheri – buheri afya
12. Buriani – buriani dawa
13. Hujambo? – sijambo
14. Umeshindaje? – salama
15. Umeamkaje? – salama
16. Habari za kutwa – njema/nzuri
17. Hongera kwa – asante nimehongea ushindi
18. Pole kwa ugonjwa – asante nimepoa
19. Lala salama – pia nawe / wa salimini
20. Kwaheri ya kuonana – kwaheri ya kuonana
21. Tuonane tena – Inshallah / Mungu akipenda
22. Makiwa – asante tunayo / asante yamepita
23. Karibu tule – starehe
Muhtasari
a) Wakati wowote
Habari? Nzuri
U hali gani? Njema
Waambaje? Sina la kuamba
Hujambo? Sijambo
Shikamoo? Marahaba
b) Asubuhi
Sabalkheri? Aheri
Umeamkaje? Salama
c) Wakati wa jioni
Umeshindaje? Salama
Masalkheri? Aheri
d) Kuagana
Kwaheri ya kuonana Kwaheri ya kuonana.
Tuonane tena Majaliwa