KILIMO

         



                           
 Kilimo ni kazi ya kulima na kupanda mazao shambani. 
Pia huitwa zaraa.


ifuatayo ni mifano ya misamiati ya kilimo.

Shamba– ardhi iliyolimwa na kupandwa mazao. 
Pia konde.
Weu-kipande cha ardhi kilicholimwa na kutayarishwa ili
kupanda mbegu au miche.Pia huitwa uchele.
Chanjaa-sehemu ya ardhi ambayo haijalimwa.
Kitalu – sehemu ya kukalishia mbegu.
Atika -kung’oa mche na kuupanda sehemu nyingine.Pia
pandikiza.
Kitivo-sehemu ya ardhi yenye rutuba.
Kiunga-shamba lenye miti mbalimbali ya matunda
Bustani-kiunga cha kupandia miti ya maua, matunda au mboga
Kwekwe– mmea uotao pasipotakikana. Pia magugu.
 Kimbugimbugi-aina ya magugu yenye urefu upatao
 futi moja mbegu ndogondogo.
Koongo – shimo dogo linalotumiwa shambani kusia mbegu.
Mche-mmea mchanga.
Tuta- mwinuko mrefu wa udongo uliotifuliwa ili kupanda
mbegu au mimea kama vile viazi.
Kufyeka – kukata na kuondoa nyasi na miti.
Kung’oa visiki – kuondoa visiki ardhini.

Ponoa-vuta ili kutoa takataka au magome kwenye mti au
mkonge.

Sekua-ng’oa kwa nguvu mmea pamoja na mizizi yake.

Pukuchua-ondoa chembe za mahindi katika gunzi kwa kutumia
mikono. Pia Pukusa.
Kulima sesa- kulima ukilainisha udongo.
Kupalilia-kulima uking’oa kwekwe au magugu.
Piga jelbe-palilia.
Kupanda sia– kupanda mbegu bila kutayarisha makoongo.
ya matunda.
Pogoa– kuyakata na kupunguza matawi ya miti.

Pukusa-angusha matunda,maua au majani kwa kutikisa mti au
mmea.Pia pukuta.

Pura-rusha jiwe au fimbo kwa nguvu kulipiga tunda lililo juu
onde.lipate kuanguka.
Pupua-ondoa majani kwenye mmea kwa kuyavuta kwa
mkono.Pia pura.
Lima ujima-lima pamoja na kwa wingi.
Ghila -mapato yatokanayo na mazao shambani.

Limbua-kula kwa mara ya kwanza mazao ya shamba au bustani
katika msimu fulani.


 Samadi – kinyesi cha wanyama kitumikacho kama mbolea
shambani.

 
Mboji– udongo ulio na rutuba ambao huchanganyika na majani
yaliyooza.Pia matanda.
Dimba-shamba lililoachwa na kurudiwa tena.

Kiamo-maziwa ya kwanza ya mnyama baada ya kuzaa.Pia
dang’a, tamari.

Chalo-shamba au konde la miwa.

 Nyunyizia – mwagilia maji kwa utaratibu.

 Kuvuna – kutoa mazao ya mimea shambani.

 Mbolea – samadi, majani yaliyooza au chumvichumvi
zitumwazo kurutubisha ardhi.

 
Rutuba – ardhi iliyo na virutubisho au mbolea ya kutosha
kuwezesha mmea kuota upesi bila tatizo lolote.

Mlimbuko– mazao ya mwanzoni wakati wa kuvuna.

 
Mrao-msimu wa mavuno wakati wa kipupwe.

 Mzao
-msimu wa mmea fulani kutoa mazao.

Gumba-hali ya kukosekana mazao ya vyakula mpaka ikaleta
shida ya watu kufa njaa.

Lima kishoroba-lima kisehemu kidogo na chembamba.

Pembejeo-vitu k.v mbegu, dawa na mbolea kwa ajili ya kilimo.



Hatua za kutayarisha shamba ni:-

Hatua za ukuaji wa nazi ni:-
Kokochi→ Kidakakitale-dafu-koromanazi.
Tanbihi:
Dunduka ni nazi inayokaribia kuwa koroma na kuoza

Kufyeka – kung’oa visiki -> kulima  »  kupanda mbegu  –  kupalilia
(kutoa magugu/kwekwe)->kunyunyizia dawa-kuvuna-→kuhifadhi.
Hali ya mimea ni:-

Ota-chipuka  -»  nawiri-komaa  -→vuna-sinyaa-kauka.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *