Masharti ya kisasa







Image result for tumbo lisiloshiba




MUHTASARI
Kisa hiki kinahusu
Kidawa, mwanamke mrembo ambaye alipendwa na muuza samaki aitwaye  Dadi.
Dadi alimpenda sana Kidawa na akataka amchumbie awe mkewe. Kidawa alimkataa
Dadi na kumkwepa kabisa. Hata hivyo, mambo yalibadilika ambayo yalimshangaza
sana Dadi. Kidawa  alimwambia kwamba yu radhi  kuolewa  na 
Dadi kwa  masharti ya ndoa  ya kisasa. Dadi kwa  shangwe
alizonazo hakuzingatia undani  wa Kidawa, ” Ujue kwamba mimi ni
mwanamke wa kisasa, na  mwanamke wa kisasa hutafuta mwanamume wa kisasa
mwenye mapenzi ya kisasa (uk 58).
Dadi akamwoa Kidawa
mwanamke wa kisasa. Baadhi  ya mambo aliyotakiwa kuyatekeleza ni kusaidia
kazi za nyumbani, kukuna  nazi, kuosha vyombo, kufua na kupiga  pasi.
Pia amruhusu Kidawa afanye kazi ya umetroni katika shule ya wasichana usiku.
Kidawa alifanya kazi  hio  kwa  zamu.  Aidha 
kidawa   akawa  na  biashara  ya  kutembeza 
bidhaa  za  Uarabuni   mitaani.  Kidawa 
aliyafanya  haya   ili “Kuunganisha ncha  nyingi za
mahitaji  ya maisha” (uk 61). Baada ya miaka  tisa ya ndoa, Dadi
alianza kuingiwa  na shaka. Akamshuku Kidawa, akachukia kujipamba kwake,
akachukia kwenda kufanya  kazi usiku, akachukia alivyosimama na kuongea na
wanaume wengine na vile vile akachukia uchuuzi  wa bidhaa alizofanya.
Furaha  ile ya kumwoa Kidawa hadi akaitwa Dadi kichekacheka kwa kumpata
mke wa kisasa Kidawa ikamtoka. Chakula kikamshinda jioni moja. Masharti ya
kuosha vyombo kwa zamu  pia yakamshinda.
Dadi  alimfuata
Kidawa  kazini  ili kumfumania na  mwalimu 
 mkuu  kama   alivyoshuku. Dadi  akaenda nyumbani
kwa  mwalimu   mkuu akaelezwa hakuwepo. Dadi akawa na
hakika  ya kuwa  mtego wake  ungenasa. Mpango wake  wa
awali alivyopanga — akapanda paipu inayoelekea gorofani ili amwone
mwalimu  mkuu  na  Kidawa  wake.  Dadi alikosea
mwalimu  alikuwa  peke  yake  na  rundo  la
karatasi akisahihisha. Kidawa alipojitoma ndani alitaka  kujiuzulu kazi
kwa kuwa mumewe anamshuku.
Dadi alionekana juu ya
paipu kisha sauti zikaanza kuuliza, “Wewe nani? Unachungulia nini
hapo  juu? Wewe mwizi, nini? Au mpiga  bodi… Nyinyi walinzi bwenini
kuna mtu amepanda juu ya papau anachungulia ndani,” (uk- 68). Sauti 
iliwavutia Kidawa na mwalimu  mkuu.  Dadi aliangukia kokoto  na
damu ikamtoka kichwani.  Kidawa alipata ni mumewe. Mwalimu mkuu akapiga
simu kuita ambulensi.

MAUDHUI
Migogoro 
ya wanandoa
· 
     Kidawa  alijua  mabadiliko  yaliyomo 
maishani.  Ingawa  wanaume wengi  walimtaka  yeye 
aliahiri  yule  atakayefuata masharti  yake. 
Alimtaka  Dadi  atoe   uamuzi.  Dadi 
alitoa   uamuzi  bila  kuelewa  kwa 
undani.   Kutokana  na  hayo  kukaingia kutoaminiana.
Ukale aliokuwa  nao Dadi, na desturi za kitamaduni zikaleta mgongano.
Laiti angalijua.
· 
     Kidawa alikuwa  mwaminifu na kwake  angetulia.
Masharti ya kisasa aliyotoa  Kidawa yalikuwa pia mageni kwa jamii. Dadi
alihisi dunia inamcheka.
· 
     Mtu anaposhuku kitu,  ni vyema  kutafuta njia
nzuri  na  salama  ya upelelezi.  Njia aliyotumia 
Dadi ya kupanda paipu ilikuwa ya kubahatisha na kudhani  kuwa
hangeonekana. Kwa sadfa alioneka.
· 
     Mgogoro unaibuka pale ambapo Dadi analazimika kufanya 
kazi za nyumbani kama  vile kukuna  seruni, kukuna  nazi na
kuosha vyombo.  Dadi anaona kuwa hizi ni kazi zinazostahili kufanywa na
mkewe.
Ahadi maishani
· 
     Kidawa alijua anataka maisha ya aina  gani na akafanya
uamuzi wake.  Aliamua  kuwa  mume atakayemuoa ni lazima afuate
masharti ya kisasa.
· 
     Dadi anapewa masharti na anayakubali. Alijitahidi sana
kuyashikilia kwa miaka  tisa. Hata akakubali kwamba wapate mtoto mmoja
kufuatilia  usasa.
· 
     Kwa Dadi hakuyaelewa yale masharti vyema  baadaye
yanamletea karaha na maisha yake yakavia.
Elimu
· 
     Elimu ni muhimu maishani. Kutokana na mwanga wa elimu mtu
husika anapata maarifa na ujuzi wa kupanga maisha yake.  
· 
     Kidawa  alimaliza   kidato 
 cha   nne   na  akatumia  ujuzi 
wake   kuandaa  maisha.  Kuna  wanaume 
wengi   waliomtaka, akawakataa na kumfuata Dadi ambaye
alimkubali.  “Wewe nimekupa mitihani mingi, na naona umefaulu”
(uk 58).
· 
     Kutokana na elimu duni ya Dadi, anaingiwa na shaka na
kumshuku mkewe. Akaona kwamba japo hajasoma, amebaini kuwa Kidawa anamwendea
kinyume.
· 
     Ukweli kwamba Kidawa ni metroni na anaenda kazini usiku, na
usiku, kukamzidishia Dadi fikra zake hizo Mume wake anafanya kazi ya kuuza
samaki.
Umbea na
masengenyo
· 
     Dadi  alihofia   minong’ono  ya 
watu   ambao  walikuwa   wanamsema  kwa 
vile  alisaidiana  na  mkewe. Jambo  hilo likamnyima 
raha. 
· 
     Wanawake na wanaume walimsema kuwa alidhibitiwa  na
Kidawa. Jambo hilo linamwumiza mno. Walidai sio mwanamume tosha.
· 
     Dadi anapozungumza na  Zuhura 
anajishikilia  ili asimpashe  maneno makali  akijua 
kuwa  bibi huyo  ni mmbea.
Itikadi/Desturi/Utamaduni
· 
     Kukuna nazi? Dadi anachukulia kuwa mwacha mila mtumwa.
· 
     Anaamini  kuwa baadhi ya kazi kama  kukuna 
nazi, kupika ni za kufanywa na wanawake.
Mapenzi  ya
dhati
· 
     Dadi alimpenda mno  Kidawa, hata  alipopewa
masharti ya kisasa pindi wakioana aliyakubali  bila kufikiria kwa makini
maneno hayo.
· 
     Baada ya miaka  tisa anashindwa kushikilia masharti,
akajiumiza bure bilashi akitafuta ithibati.
· 
     Kwa upande wa  Kidawa  naye,  alikuwa 
na  mapenzi  ya  dhati.  Wanapotembea njiani 
alimkemea  Dadi  —  hakutaka kuangalia wanawake wengine.
Anapojipamba vyema alimwuliza  mumewe ikiwa amependeza.
· 
     Kidawa  kufuatwa na  wanaume wengi  waliomtaka 
uchumba,  waliosoma  na  wasiosoma,  wenye 
uwezo  na  wasio  nao  lakini anawapeperushwa wote nje ya
unyumba wa ndoa  na kumkubali  Dadi (uk. 57 – 58).
· 
     Mwalimu mkuu kuwa mwaminifu kwa mkewe.
· 
     Kidawa kuwa mwaminifu kwa mumewe licha ya mumewe
kutomwamini.
WAHUSIKA
Dadi
Huyu
ni mchuuza samaki. Alimpenda mwanamke mmoja (Kidawa)  kupita  kiasi.
Dadi alijaribu  kumpata Kidawa  kwa  kila njia  lakini
hakuweza. Alikata tamaa kabisa. Kidawa alibadilisha mtazamo wake. Dadi akapewa
masharti ya kisasa katika ndoa  yao. Masharti hayo yanamuumiza rohoni na
kumsononesha.
· 
     Ana bidii: anachuuza samaki kwa bidii hadi wamalizike.
· 
     Kigeugeu: anayumbishwa na maneno ya watu hadi akakosa raha
kabisa.
· 
     Mvumilivu – anavumilia mitihani mingi aliyopewa na Kidawa
kabla ya kukubali uchumba wake.
· 
     Mchangamfu – baada ya uchumba wake kukubaliwa na Kidawa,
anaanza kuwa na tabia  ya kutabasamu na kuchekacheka hata pasi na kuweko
kitu cha kuchekesha hadi watu wakamlakabu Dadi Kichekacheka (uk. 58 – 59).
· 
     Mwenye   mapuuza –  anajifunga 
kukubali   masharti  ya  kisasa  licha 
 ya  kutojua   maana  ya  masharti 
yenyewe.   Anaishia kutoyazingatia masharti hayo vyema.
· 
     Mwenye shauku/mashaka- anashuku kuwa mkewe  anamwendea
kinyume na mwalimu  mkuu.
· 
     Mwenye taasubi – anakeketeka maini akifikiri kuwa
ataonekana na wanawake na wanaume mtaani kuwa yeye si mwanamume tosha kwa
kutiwa maganjani na kudhibitiwa  na mkewe.
· 
     Mkali – anakasirika Bi. Zuhura anapomwambia ati samaki wake
wameoza. Anachupia baiskeli yake na kuondoka.
· 
     Mdadisi/mchunguzi  – anafanya  uchunguzi 
mkali  kuhusu  nyendo   za  mkewe, 
anamfuata  hadi   mahali   pake   pa 
kazi  na kuchungulia dirishani.
Umuhimu
· 
     Kupitia kwake  tunajua  kuwa  si  vizuri
kuzingatia  tuhuma kabla  ya kuhakikisha;  sio 
rahisi  kuleta  mabadiliko  katika  jamii. Ametumiwa
kutonyesha shida zinazosibu wanandoa wa leo.
Kidawa
Mwanamke
mrembo ambaye alitongozwa na wanaume wengi. Aliwakataa na kuwachuja hadi
akamchagua Dadi. Yeye alisoma hadi kidato cha nne. Alitaka mwanandoa ambaye
angezingatia masharti ya kisasa ya ndoa.
· 
     Ni mzingatifu: anajua alitaka  nini maishani na
akazingatia matakwa yake — ya ndoa  ya kisasa.
· 
     Ni jasiri: Hakuyumbishwa na umbeya wa wanajamii kama 
Dadi.
· 
     Mbaguzi  – anawabagua wanaume wengi; waliosoma na
wasiosoma; walio na uwezo  na wasiokuwa nao na kumkubali  Dadi
· 
     Mjasiriamali – kando  na kazi yake ya umetroni,
anafanya kazi nyinginezo kama  kutembeza bidhaa ili kuongeza pato 
lake.
· 
     Mkaidi – mumewe anawazia kumkataza kutembeza bidhaa, hasa
nyakati  za usiku, lakini anachelea kufanya  hivyo kwa kujua kuwa
Kidawa hakataziki.
· 
     Mwenye   kinyongo/ghere  – huwa 
 anamkemea  mumewe  kwa  kuwaangalia  wanawake 
waliovaa   mavazi   yanayowabana.
· 
     Hupenda kubwata, “stop your gaze!” (uk. 65). Pia anapenda
kujipodoa na kuvaa  vizuri ili mumewe asije akaanza kuwa na jicho la nje.
· 
     Mbinafsi – anajipamba ili kufurahisha moyo wake bila kujali
kovu analomwachia mumewe (uk. 66).
· 
     Mwaminifu – licha ya mumewe kutomwamini, hamwendei kinyume
na mwalimu  mkuu.
· 
     Nadhifu – anapenda kuvaa mavazi  nadhifu, kujipodoa na
kujirashia marshi mazuri.
 Umuhimu
wake
·       Kidawa ni kielelezo  cha
mwanamke wa kisasa ambaye hataki  kushikilia mila za kizamani. Kupitia
kwake, tunausiwa kuwa ni vyema mtu atoe  msimamo wake maishani ili
ujulikane bayana.
 Mnunuzi wa samaki
  Ni Bi. Zuhura.
·       Mwenye maneno ya karaha –
Anakashifu samaki wa Dadi na kudhani  kuwa wameoza.
       Ni mmbeya: anampiga Dadi
vijembe kujua kuhusu jinsi anavyoindesha ndoa  yake.
Umuhimu Wake_ 
 Ni kiwakilishi cha wanawake wambeya wanaojiingiza kwenye mambo ya watu.
Mwalimu Mkuu
·       Ni mwalimu  mkuu 
wa shule ya wasichana anapofanya kazi Kidawa. Ameaoa.
·       Mara nyingi huwa 
afisini mwake hadi usiku akizipinguza kazi zake.
·       Mwenye utu: anapiga simu
mara  moja kuita ambulensi baada Dadi kuanguka na kuumia  kichwani.
·       Mwaminifu – hana 
uhusiano wa kimapenzi na Kidawa licha ya kwamba alikuwa anatumia muda mwingi
naye hata  wakati wa usiku.
·       Mchapa kazi – hubaki afisini
hata  majira ya usiku ili kupunguza kazi zilizomsonga.
MBINU ZA UANDISHI
Taharuki
·       Baada ya kupelekwa hospitali,
Je alipona au aliaga dunia, ukizingatia kuwa aliumia vibaya kichwani.
·       Je, Kidawa alikichukuliaje
kitendo hicho cha mumewe kupanda juu ya paipu na kuchungulia ndani?.
Taswira
·       Baada ya Dadi kupelekwa
hospitalini, Je, alipona au aliaga  dunia? Ukizingatia kuwa aliumia vibaya
kichwani.
·       Je, Kidawa alikichukuliaje 
kitendo  hicho cha mumewe kupanda juu ya paipu na kuchungulia ndani?
·       Je. Hatima  ya
ndoa  ya Kidawa na Dadi ilikuwa gani? n.k.
·       Taharuki  inaibuka 
Dadi anapoanza kumshuku mkewe. Je, ni kweli kuwa  mkewe  anamwendea
kinyume  na mwalimu mkuu?
·       Taswira ya Dadi akiwa juu ya
baiskeli yake akiita wanunuzi.
·       Kuna taswira ya Kidawa akiwa
amevalia viatu vipya na kanzu  tayari kwenda kazini usiku.
·       Aidha kuna taswira ya kile
chakula cha jioni cha ndizi na samaki ambacho Dadi hakukigusa
Sadfa
·       Dadi alienda 
kuona  iwapo  mwalimu  alikuwa  kwake  jioni.
Alipomkosa  akajihakikishia  kwamba alienda  kukutana na Kidawa.
Anaenda afisini na kuwapata wakiwa pale.
·       Aidha ilikuwa sadfa kuwa taa
ya nje ilikuwa haiwaki na Dadi akapata mandhari mazuri  ya kujificha
akipanda ile paipu.
·       Siku ile Dadi anapoenda
afisini  kuchunguza nyendo  za  mkewe  ndiyo 
siku  mkewe  anapoacha kazi  kwa  sababu ya mumewe
kutomwamini (uk. 68).
·       Mahali pale  ambapo Dadi
alipata paipu  na kuiparamia palikuwa  mahali  ambapo hapakuwa
panapitwa na watu  sana.
·       Ni sadfa kuwa usiku ule Dadi
anapokuja pale ndipo walipita watu wakamwona akiwa pale juu.
Kuchanganya
ndimi
·       Kuna maneno ya Kiingereza
yaliyotumika  kama  “Stop your gaze!”
·       my dress my choice  ·       celeb      socialite n.
Mdokezo
·       Kidawa  alijaribu 
kumhakikishia  mumewe uaminifu  wake  na  kumkumbusha ahadi 
zao,  alipogeuka  na  kuona  chakula  hakikuguswa
alikatisha usemi wake (uk 66)
·       Dadi alipokuwa akienda
shuleni kumwangalia mwalimu  mkuu, alijiapiza kuwa leo ni leo na
hakumaliza msemo huo.
·       Wakati  mwalimu 
 mkuu  alipokuwa  akimwasa  Kidawa  kuhusu kuacha
kazi,  mdokezo umetumika,  “Mtu  ana   kazi 
nanga zinapaa, sikwambii… “(uk 68)
Takriri
Neno kisasa limerudiwarudiwa kusisitiza kiini cha 
hadithii hii “Mwanamke wa kisasa hutafuta mwanaume wa kisasa, mwenye mapenzi ya
kisasa (uk 58)
·       …nyakati hizi hizi za kisasa
(uk. 58).
·       …neno ‘kisasa’ hatua kwa
hatua, kipembe baada ya kipembe (uk. 58).
·       …alijatibu kuyapinduapindua,
kuyapekuapekua na kuyabiruabirua ilia pate…
·       Roho haitaki, na ikiwa roho
haitaki ndio haitaki (uk. 64).
Tanakuzi
·       Tanakuzini matumizi ya maneno
yanayopingana.
·       Waliosoma na wasiosoma
·       wenye uwezo  na wasio
nao (uk 57)
Majazi
·   
   Kidawa –
ni dawa  la mapenzi ya Dadi
·       Dadi– dadisi. Kuulizauliza na kufanya  uchunguzi. Anadadisi
kuhusu nyendo  za mkewe
Sitiari/jazanda
·       …anafuata nyuki apate kula
asali… (uk. 56). Nyuki hapa ni Kidawa na asali ni mapenzi ya Kidawa.
·       Dadi akageuka maji ya kuuzima
moto… (uk. 57). Maji hapa ni Dadi na moto  ni Kidawa.
Utohozi
·       …katia saini…  ·       …paipu…
Sauti
· 
     Hujitokeza pale hadithi inapokuwa na sauti ya mtu, kitu au
mnyama. Sauti hiyo huchangia katika kukuza  vitushi vikuu vya hadithi.
· 
     Pom poom! Pom poom! Pom poom… (uk. 59). Sauti ya honi ya
baiskeli ya Dadi ikiita wateja.
· 
     Kuna sauti  ya wapita  njia wanapomwona Dadi.
· 
     Sauti  hiyo inauliza  anachofanya 
pale  juu;  ikiwa anawachungulia  wasichana; inamshtumu yeye
kuwa mpiga  bodi; inamshtumu kuwa mwizi; inaita walinzi wa bweni waje
wamwone mtu aliyepanda pale juu;

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *