MAJINA YA UKOO/NASABA

kalonzo musyoka,wcb,misukosuko,majanga,mlemavu,mama mlemavu,mwanamke mlemavu,story za kijamii,magufuli,makonda,wasafi tv,ayo tv,lobal tv,habari,azam tv,bbc news,bbc swahili,ramani,abrahamu,historia ya mtu,mweusi,millardayo,majina,utumwa wa mtu mweusi,kwaresma song,church,jesuslovesyou,lord,grace,photography,worship,kwaresma,kwaresma 2019,kwaresma nyimbo,nyimbo mpya 2019,crucifixion,nyimbo za kwaresma,nyimbo za dini
MSAMIATI WA UKOO


        Msamiati wa ukoo ni majina wanayoitana watu walio na uhusiano wa kidamu au watu walio katika familia moja.Ukoo pia huitwa nasaba ,mlango au jamaa.
Utamaduni wa Mwafrika umejaa heshima na adabu .Hivyo basi,watu mbalimbali katika jamaa huitana majina maalum kudhihirisha heshima na adabu.

Yafuatayo ni majina ya ukoo:

Ahali -Mke.
Ajinabi-mtu ambaye hahusiani nawe kiukoo ambaye unaweza kumwoa.
Arusi-hali ya mwanamume kumchukua mwanamke kisheria na kukaa naye kuwa mke
Arihami – jamaa wa damu hasa kwa upande wa kuukeni.
Ami-Ndugu wa kiume wa baba, Pia amu.

Baba -Mzazi wa kiume. Pia abu.
Buraa -samehe mahari ili kupata talaka.Pia Bihi.
Bin– Mtoto wa kiume wa k.m Evans Bin Mokua
Binti-mtoto wa kike wa.Pia biti k.m Joyce Binti Makone
Babu-Mzazi wa kiume wa baba au mama.
Binamu -Mtoto wa kiume wa ami, shangazi, halati, mjomba.

Baba wa kambo -Baba mlezi asiye baba mzazi.
Baba wa kupanga -Mwanamume amleaye mtoto ambaye si wake wala wa mkewe.

Bintiamu -Mtoto wa kike wa ami, shangazi, halati, mjomba.
Bavyaa –Baba wa mume wako..
Dada – Ndugu wa kike.
Halati -Ndugu wa kike wa mama. Pia hale.

Ingia mafa
– rithi mke wa ndugu kwa kumwoa.

Kuumeni -Ukoo wa upande wa baba.

Kifungua mimba -Mtoto wa kwanza kuzaliwa. Pia  Chudere au mwanambee 
Kitinda mimba -Mtoto wa mwisho kuzaliwa. Pia mziwanda au kichinja mimba.
Kitukuu -Mtoto wa mjukuu. Pia mtukuu.
Kilembwe -Mtoto wa kitukuu.
Kaka– ndugu mkubwa wa kiume.Pia nduga wa kiume.
Kijana-Msichana au mvulana kati ya miaka kumi na minane hadi thelathini na mitano. Pia Kijulanga.

Kilembwekeza –mtoto wa kilembwe. Pia kinying’inya au kining’ina.
Kivyere -Jina waitanalo wazazi wa mume na wazazi wa kike
Kuukeni – ukoo wa upande wa mama.
Kizuka -Mjane wa kike.Pia mfaruku au mfarukwa.

Mnuna -Ndugu mdogo.
Mama-Mzazi wa kike.Pia nyina.
Mhale -Mume wa halati.
Mkazamjomba -Mke wa mjomba.
Mpwa -Mtoto wa dada au kaka yako.
Mkoi -Mtoto wa ami, shangazi, halati au mjomba. Hivyo basi, mkoi anaweza kuwa bintiamu au binamu.
Mjukuu -Mtoto wa mtoto wako.
Mkwe –Mzazi wa mkeo. Pia mcheja.
Mama wa kambo -Mama mlezi asiye mama mzazi
Mama wa kupanga- Mwanamke amleaye mtoto ambaye si wake wala wa mumewe.
Mke mwenza -Jina waitanalo wake wawili au zaidi waliooleka na mume mmoja.
Mtala -mke mmojawapo miongoni mwa wake wa mtu mmoja.
Mitara-ndoa ya wake wengi.Pia mtala.
Mwanyumba –Waume waliooa dada wawili au zaidi katika boma moja.
Mhavile-Mume wa shangazi.
Mkazaamu -Mke wa amu.
Mkazamwana– mke wa mwana.
Mjomba -Ndugu wa kiume wa mama. Pia hau.

Mkwerima -Jina analotumia mzazi wa mke kumwita mume wa binti yake.

Mavyaa-Mama wa mume wako.
Mwamu -Ndugu wa kiume wa mkeo.Pia mlamu au muamu.
Mwana
-Mtoto wako.
Mwana harashi -Mwana aliyelaanika au asiye na adabu.
Mtalaka-mume au mke aliyeachana na mwenzake
Maharimu – mtu usiyeweza kumwoa au kuolewa naye kwa sababu ya uhusiano wa nasaba k.v ndugu wa tumbo moja.
Ndugu-Watoto waliozaliwa tumbo moja
Ndugu mlungizi-Ndugu anayekufwata nyuma.
Nyanya-Mzazi wa kike wa baba au mama.
Pacha-Ndugu wawili au zaidi waliozaliwa tumbo moja na wakati mmoja.
Sagai -sherehe ya kukutanisha upande wa mume na wa kike baada ya posa kukubaliwa ili kuonesha ishara ya kuukeni kumkubali na kumpokea bwana harusi.
Sora-chukua mwanamke kwa makubaliano bila ya kufunga ndoa.
Shangazi-Ndugu wa kike wa baba. Pia Amati au mbiomba au shambazi.


Ubuni -nasaba ya upande wa baba kwa mtoto wa kiume.
Umbu -Jina waitanalo dada na ndugu yake wa kiume au kaka na ndugu yake wa kike.

Ujombani-upande wa mama kinasaba.

Wifi -Ndugu wa kike wa mumeo.
Yatima -Mtoto aliyefiwa na wazazi wake wote. Pia kiokote ,makiwa au mwanamkiwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *