VIBADALA

VIBADALA

Kibadala ni neno linalotofautiana kidogo na neno jingine
kimatamshi lakini lenye maana sawa.

Mifano ya vibadala

 Alfeni -elfeni
 Alfu -elfu
Arusi -harusi
Angalao -angalau
Afisa -ofisa
Blanketi -blangeti
Barobaro -barubaru,
Banki -benki
Bakara-bakari
Bufeti -bufee
Chakuleti-chokoleti
Darahimu -dirhamu
Desturi -dasturi
Disemba -Desemba
Ekari-Eka
Faraji-faraja
Firauni-farao
Fikra-fikira
Guruneti-gruneti
Gulamu-ghulamu
Gagulo-gagro
Haleluya-aleluya
Jumuiya-jumuia
Jagina-chagina
Kabeji-kabichi
Kibiongo-kibyongo
Kichinjamimba -kitindamimba
Kilabu-klabu
Kuwadi-guwadi
Kiza-giza
Kumradhi-kunradhi
Laazizi-azizi
Malaji-maakuli
Maleba-maleva
Mharage -mharagwe
Minghairi ya -bighairi ya
Mwizi -mwivi
Mathalani-mathalan
Maamkizi -maamkio
Machela -machera
Majaliwa-majaaliwa
Ninyi -nyinyi
Ndoana -ndoano
Pembea -bembea
Peta -pepeta
Ramba -lamba
Rowa -lowa
Sufuri -sifuri
Surua -shurua
Shimizi-shumizi
Shukrani-shukurani
Taka-takataka
Takariri -takriri
Tarabushi -tarbushi
Tubwi -chumbwi
Tingisha -tikisa
Trela -tela
Rasilmali-rasilimali
Pirikapirika-pilkapilka
Ubongo -bongo
Umbea-umbeya
Uwele-uele
Vunjajungu-kivunjajungu
Wadi-wodi
Mvyere -mvyele
Nambari -namba
Waridi-alwaridi
Yumkini-yamkini
Zaibaki -zebaki
Zungurusha -zungusha

USHAIRI

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *