Msamiati wa wafanyakazi



msamiati,mwendeleo wa kiswahili,mawasiliano na uchukuzi,matukio ya tanzania,taarifa tanzania,habari za tanzania,namachanja high,mwananchi,palinyang gabriel,wasafi,dalmus sakali,mafunzo,matamshi,rc aggrey mwanri,habari za kila siku,habari mpya,fyeka,jifunze,maelekezo,thecitizen,msarifu bin bashashi,west tv kenya,bei ya mafuta,dawati la lugha,mange,tabora,habari,kimambi,interview,supreme court,lands ministry,na,vat,ardhi,chali,marco,konki


Msamiati wa wafanyakazi 

Kazi ni shughuli yoyote halali afanyayo mtu ili kukimu mahitaji yake.Watu
hupata kazi hizo kutokana na masomo yao au tajriba na uzoefu.
Mifano ya wafanyakazi:
Tabibu – Mtu aliye na utaalamu wa kuwatibu wagonjwa.
Dereva – Mtu anayeendesha gari.
Bawabu – Mtu anayelinda lango.
Muuguzi au nesi– Mtu anayemsaidia daktari kuwapa wagonjwa dawa na kuwatunza.
Tarishi au katikiro– Mtu anayefanya kazi ya kutumwa katika ofisi ili kupeleka barua.
Mhasibu – Mtu anayetunza pesa katika kampuni.
Msajili – Mtu anayeweka orodha na habari za mambo mbalimbali.
Hamali – Kibarua ambaye huwachukulia watu wengine mizigo kwa malipo.
Sogora- Fundi wa kucheza densi au kupiga ngoma.
Mhandisi – Mtu mwenye maarifa na ujuzi wa kuunda na kutengeneza mashine. Fundi wa mitambo.
Sonara – Fundi wa kutengeneza mapambo ya dhahabu.
Nahodha – Mtu mwenye utaalamu wa kuendesha meli.
Kuli – Mtu anayepakia au kupakua mizigo melini.
Msusi – Mwenye ujuzi wa kusuka.
Mshenga – Mtu atumwaye na mwanamume kupeleka posa kwa wazazi wa mwanamke.
Mvuvi – Mtu anayevua samaki.
Dobi – Mtu anayefulia watu nguo kwa malipo.
Mhariri – Mtu anayefanya kazi ya
Dobi– Mtu anayefulia watu nguo kwa malipo.
Mhariri- Mtu anayefanya kazi ya kusoma, kusahihisha na kusanifu maandishi ya vitabu, majarida au magazeti.
Mkutubi-Mwenye ujuzi wa kuhifadhi vitabu na kuendesha maktaba.
Rubani– Mtu anayeendesha ndege.
Kinyozi Aliye na ujuzi wa kuwanyoa watu nywele.
Kasisi– Kiongozi wa dini ya ukristo aliyepewa daraja la kuendesha misa. Huitwa pia padri.
Saisi-Mtu anayemtunza na kumpanda farasi.
Imamu– Kiongozi mkubwa wa  Waislamu anayeongoza sala ya pamoja.
Dalali– Mtu anayeuza bidhaa mnadani.
Mkadamu- Msimamizi mkuu wa mashamba.
Nokoa- Msimamizi wa mashamba aliye chini ya mkadamu.
Mhunzi– Mtu anayefua vyuma.
Mwashi – Mtu mwenye ujuzi wa kujenga nyumba kwa mawe.
Seremala– Mtu anayetengeneza vitu kwa kutumia mbao.
Mfinyanzi – Mtu anayetengeneza vyombo kwa kutumia udongo.
Diwani– Mtu anayechaguliwa na wakazi wa eneo fulani ili awawakilishe katika halmashauri mji, jiji au wilaya.
Topasi au chura – Mtu afanyaye kazi ya kusafisha vyoo.
Mzegazega – Mtu anayeuza maji kwa kuyatembeza.un
Utingo – Mtu anayepakia au kupakua mizigo katika matwana.
Ngariba – Mjuzi wa kuwatahiri wavulana jandoni.
Mkalimani – Anayetafsiri habari kutoka lugha moja hadi nyingine.
Malenga – Mtu mwenye ujuzi wa kutunga mashairi.
Manju – Mtaalamu wa kughani mashairi.
Mhazigi – Daktari wa kuunganisha mifupa.
Serehangi– Msimamizi wa mabaharia.
Mchuuzi– Mtu anayeuza bidhaa kwa kuzitembeza.
Mutribu- Fundi wa kupiga ngoma.
Mpishi – Mtu aliye na ujuzi wa kupika vyakula.
Msukaji – Mtaalam wa kusuka mikeka au vikapu.
Mwezekaji – Mtu mwenye utaalamu wa kuezeka mapaa ya nyumba.
Mkunga – Mtu anayewasaidia kina mama wakati wa kujifungua.
Yaya – Anayefanya ya kuwalea watoto.
Mhazili – Anayefanya kazi ofisini kuandika habari kwa taipureta au kwa kompyuta.
Kocha – Mwalimu wa mpira au riadha.
Mhadhiri – Anayetoa mhadhara katika chuo kikuu au mbele ya watu.
Kungwi-Anayefudisha vijana wa kike waliobaleghe mambo ya unyumba.
Refa au refari– Mtu anayefanya uamuzi kwenye mchezo.
Msasi-Mtu ambaye kazi yake ni kuwinda wanyamapori mwituni
Jangili-Mtu anayewinda wanyama pori kinyume cha sheria
Kandawala-Anayeendesha gari moshi
Mjumu-Mtu anayefua visu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *