Vitate ni maneno yanayotatanisha kwa sababu ya ukaribu uliopo kimatamshi na kimaendelezo baina yake.
Mifano ya vitate:
Wasiwasi-jakamoyo, wahaka au shaka.
Waziwazi-bila ya kuficha.
Dhamini-wekea mtu ahadi kuwa utatimiza jambo fulani.
Thamini-tia maanani au heshimu.K.m Asiyekujua hakuthamini.
Bamba-lazimisha mtu kufanya ngono naye.
Pamba -chakula cha wakati wa safari.
-tia urembo au visha mavazi mazuri na ya kupendeza.
Bali-isipokuwa, lakini, ila.
-tia maanani.K.m sijali wala sibali atakayosema
-herini.
Bari-jitenge,kaa kando
Mbali-masafa marefu baina ya mahali na mahali,
hatua kwa hatua au mwendo mrefu.Pia umbali.
-sio sawasawa.Pia tofauti k.m shati hili lina rangi mbali na lile.
-Kwa kitambo kirefu k.m Amekwenda mbali.
Mbari -Watu wa kitovu kimoja.Kabila au ukoo.
Chini -Kinyume cha juu.
-ndani ya ardhi,pango au meli.
-sehemu ya mbele kinenani.Pia tupu.
Sini-udongo maalum wa kutengeneza vyombo.
-asilani! au abadani!
Zini -kutenda tendo la kujamiana bila kufuata taratibu za kidini
Bua-shina la mtama au mhindi.
-hutumika katika usemi: moyo wa bua-moyo unaotishika kwa wepesi.
-chuma cha wahunzi cha kukolezea moto.
Pua-paka kitu kiowevu mwilini kwa kutandaza kiganja cha mkono.
-maliza yote bila kubakisha kitu.
-kiungo cha mnyama chenye tundu kinachomwezesha kuvuta pumzi na kunusia.
Fua-tengeneza kitu kutokana na madini.Pia sana.
-,safisha nguo kwa maji na sabuni.
-chano.
Vua-ondoa mwilini kitu kilichovaliwa.
-toa katika matatizo.Pia nusuru.
Chaka -mahali penye miti iliyosongamana.
-msimu wa kaskazi.
Shaka -hali ya kutokuwa na hakika ya jambo.Pia wasiwasi.
Posa-peleka maombi ya kutaka kuoa kwa wazazi wa binti.
Poza-malipo ya kumtuliza mtu kwa jambo baya alilotendewa.
Saka-tafuta mtu au mnyama ili kumkamata.Pia winda.
Zaka -moja ya kumi ya pato ambalo waumini wa baadhi ya madhehebu ya Ukristo hutarajiwa kutoa kwa ajili ya
shughuli za kanisa.
Suka-fuma kitu ili kupata mfumo fulani ulioshikamana.
Shuka-teremka
Zuka-Anza au tokea kwa kitu au jambo ambalo halikuwepo wala kutegemewa.
Joshi-kwa haraka k.m dau la mnyonge haliendi joshi.
-mwendo wa chombo wa kufuata upepo wa katikati
Jozi-vitu viwili vilivyopamoja na vinavyofanana.
Chozi-tone la maji au uowevu linalotoka machoni mtu anapolia au moshi unapoingia machoni
Tosa-tia kitu katika kiowevu kama mafuta,tui,maji,n.k
-tunda linalokaribia kuiva k.m Embe tosa litaliwa kesho
Toza-chukua vitu kama pesa kutoka kwa mtu kuwa ni ushuru, kodi au fidia.
Nadhari -akili nzuri.Pia busara k.m mtu aso nadhari,ng’ombe
Nathari-maandishi ya kawaida kama Insha, hadithi, tamthiliya,riwaya,n.k
Kibofu -fuko la mkojo lililoko tumboni
Kipofu -mtu asiyeona
Kibovu -kisichofaa au kilichoharibika k.m kiti hiki ni kibovu
Kobe –jina la dharau kwa mtu anayeshindwa kufunga katika mwezi wa Ramadhani.
-mnyama kama kasa mwenye magamba magumu,shingo fupi na aendaye polepole.Pia Furukombe.
Kope -nywele zilizo katika kikawa cha jicho
-ngozi zinazofunika macho wakati yakiwa yamefumbwa.
-ncha ya utambi wa taa iliyowashwa.
Chusa -chombo mfano wa mkuki wenye meno matatu cha Kuwavulia samaki wakubwa kama papa, Chewa au
nguru.
Chusha -kosa kuridhisha.Pia chukiza.
Pora-nyanganya kwa kutumia nguvu.Pokonya au bwakura.
-jogoo ambaye hajaanza kuwika.
Bora-kitu cha kufaa zaidi au chenye thamani. Pia afadhali.K.m Gari lako ni bora kuliko langu.
Shari-jambo linaloleta hasara au matokeo mabaya.
-jambo la kumwudhi mtu.Pia ugomvi au chokochoko
Shali-kitambaa cha sufu cha kuvaa begani na shehe.
Zindika -fanya kitu kuwa imara kwa kukifanyia dawa zenye kukinga madhara.K.m Kiwanja hicho
kimezindikwa dhidi ya wanyakuzi
Sindika -funga mlango au dirisha bila ya kutia komeo wala kubana. Pia Shindika.k.m Tafadhali zindika mlango ili mdogo wako aweze kuufungua.
Baba – Mzazi wa kiume.
Papa – Aina ya samaki.
Sahibu – Mwandani au rafiki.
Shahibu – Mwanamume mzee.
Dhibiti -Weka sawasawa.
Thibiti – Kuwa ya kweli au ya kuaminika.
Bibi – Mke wa mtu au nyanya.
Pipi – Aina ya peremende.
Sana– Iliyozidi kawaida.
Sanaa – Ufundi wa kuwasilisha hisia na mawazo ya kibinadamu.
Kula –Tia chakula kinywani na kukimeza.
Kura – Uchaguzi unaofanywa ili kumchagua mtu.
Samani-Vyombo vilivyotengenezwa kwa mbao
Zamani – Kitambo au miaka mingi iliyopita.
Choka – Pungukiwa na nguvu mwilini baada ya kufanya kazi.
Shoka – Kifaa cha kuchanjia kuni.
Kalamu – Kifga cha kuandikia.
Karamu –Vyakula vilivyoandaliwa watu wengi kwa ajili ya shughuli maalum.
Kua – Kuongezeka kwa umri na kimo.
Kuwa – Tendeka.
Komaa – Kuwa mtu mzima.
Koma – Fikia mwisho au hatima.
Bunda –Fungu la vitu kama karatasi au nguo
Punda – Mnyama afananaye na farasi atumikaye kubebea mizigo.
Mahari –- Malipo ya kuolewa au kuoa
Mahali – Masikani au sehemu ya mazingira.
Songa – Kusanya pamoja na kuelekeza upande mmoja.
Zonga – Zunguka kwa mambo mengi.
Sama – Sakama kooni.
Zama – Didimia majini; kale.
Bahasa – Bei ndogo isiyo ghali.
Bahasha – Karatasi iliyokunjwa inayotiwa barua.
Hanja – Zunguka huko na huko kwa majivuno
Haja – Matlaba au mahitaji.
Fuka – Toka moshi.
Vuka – Pita au enda upande wa pili.
Lia- Tokwa na machozi pamoja na sauti hasa mtu akifikwa na huzuni au maumivu.
Ria – Hali ya kufanya jambo kwa ajili ya kutaka kusifiwa.
Fara – Ukingo wa juu wa chombo cha mjazo.
Fala – Mtu aliyepumbaa
Posa – Peleka maombi ya kutaka kuoa kwa mzazi wa mwanamke.
Poza – Malipo apewayo mtu ili kumtuliza kwa jambo.
Ungua-Teketea kwa moto.
Ugua- Patwa na ugonjwa.
Fuja-Tumia mali vibaya.
Vuja– Hali ya kitu kiowevu kama vile maji kupita kwenye sehemu ndogo kama tundu.
Pima- Kukadiria ukubwa, wingi, hali au uzito wa kitu.
Bima- Mpango wa kulipa fedha katika kampuni au shirika ili kupata fidia baada ya muda fulani.
Bata– Ndege afugwaye nyumbani.
Pata – Kuwa na kitu ulichokitarajia.
Vua -Toa nguo mwilini au toa samaki majini.
Fua – Osha nguo. Tengeneza kitu kutokana na chuma.
Msasi – Mtu anayewinda wanyamapori.
Mzazi – Baba au mama.
Mchuuzi-Mtu anayeuza vitu rejareja.
Mchuzi – Kitoweo kiliwacho majimaji.
Doa – Alama juu ya kitu au kasoro.
Ndoa – Harusi au nikahi.
Picha – Umbo la kitu au mtu lililoandikwa, kuchorwa au kupigwa chapa
Pisha– Kumpa mtu nafasi ili apite
Vuta-sukuma kuja upande wako
Futa-Pangusa ondoa uchafu
Randa-Zurura
-Kifaa cha seremala
Landa-fanana k.m Anamlanda mamaye
Nchi-taifa,Jamhuri
Inchi-Kipimo cha urefu katika rula au mita
mchi-Mti wa kutwangia katika kinu
Mji-Mkusanyiko wa nyumba nyingi,maskani ya watu
– sehemu ya tumbo la uzazi kwa wanawake ,tumbo la uzazi
Masaibu-Matatizo yanayomkumba mtu
Mashaibu-wanaume wazee
masahibu-marafiki
Jabari-mwenye nguvu
Jabali-jiwe kubwa;mwamba
Fahari-utukufu au majivuno
Fahali-ng’ombe dume
Faa-kuwa na faida
Vaa-kutia nguo mwilini
Daawa-madai au jambo linalosababisha ugomvi
Dawa-Kemikali inayotibu maradhi au kitu anachopewa ili awe katika afya au mienendo mizuri
Asi-goma,kataa kufuata sheria
Hasi-Kumfanya ng’ombe dume kuwa maksai,ondoa makende kutoka kwa mnyama dume
Ama- au,pengine
Hama-hajiri
-toka katika makao fulani na kwenda kwingine
ngoma – ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa
goma –acha kufanya kazi
shindano – makabiliano baina ya watu wawili au zaidi ili kutambua atakayeongoza
sindano –kifaa kinachotumika kushonea vitu
Haba –kisichokuwa kingi
Hapa –mahali karibu