NGANO

Ngano ni ule utungo, hubuniwa kufundisha
Huelezwa kwa mpango, uweze kuburudisha
Uwe kweli na urongo, jamii hufunganisha
Mtambaji ni fanani, mwenye lugha  natharia

Ainaze ni hekaya, mazimwi yakishetani
Khurafa wanoongeya, na mashujaa fulani
Kuna za mafumbo piya, zenye maana ya ndani
Visasili mitanziko,mwisho wake ni usuli.

Wahusika wa hekaya,wakuu ni binadamu.
Wabunifu nakwambiya,wajanja walohitimu
Wachekesha ukaliya,na ushindi unatimu
Hekaya ni za kubuni,kitambiwa tashangaa.

Tukienda kwa mazimwi,wao ndio wahusika
Wakatili ja ukimwi,ila washindwa kumbuka
Sifa za hao mazimwi,zinakiuka mipaka
Wana kinywa kisogoni,jicho moja tena kubwa!

Wahusika wa hurafa,ni ndege au wanyama
Za watu nd’o zao sifa,wana funzo chungu  nzima
Kwa dhifa au maafa,ucheshi huo lazima
Ushindi hujitokeza,kwa hurafa za kijanja

Na mashujaa ni watu,wanookoa jamaa
Hawaogopi misitu, lila na fila wakaa
Tena wahimiza watu,kutoikata tamaa
Wao ndio wahusika,uhimiza uzalendo.

Tukija kwa visasili,ni hadithi fahamuni
Zinoeleza asili,ya matukio fulani
Kama kifo na ajali,kiimani na kidini
Wahusika ni wanyama,na binadamu ujue.

Mitanziko mhusika,huwa kwenye hali tete
Hali ngumu humshika,hushindwa kipi afate
Mwishowe hulazimika,kukiteuwa chochote
Wahusika ni wanyama ,na binadamu ujue.

Usuli zaelezeya,ile asili ya hali
Wasifu au tabiya,za vitu aina mbali
Mambo hasi yagusiya, kutufunda  maadili
Wahusika ni wanyama ,na binadamu wenzetu.

Wifadhiwa akilini,kichwani mwa binadamu
Diski huwekwa ndani,isipotee dawamu
Na kanda za redioni,wana wapate ilimu
Si hayo hata michoro, na video zinawekwa

 PAINKILLER MALENGA SERA

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *