INSHA

INSHA


Image result for insha

Utungo
unaoundwa kwa mfululizo wa sentensi zinazozungumzia jambo, tukio au kitu fulani
Aina
1.   INSHA
ZA KAWAIDA
a)   Insha
ya Picha
 Ambapo
mwanafunzi amepewa picha kadha na kutakiwa kutunga kisa na kueleza yote
yanayotokea kwenye picha hizo. Chunguza vizuri ujue kinachotokea katika hizo
picha.
ü  Kichwa
kiafikiane na picha ulizopewa. Kila picha ipangwe na kuwa na aya moja.
b)   Insha
ya Methali
 Insha
inayosimulia kisa kinachoonyesha ukweli au uongo wa methali Fulani.
 Wazia
methali nyingine za kutilia mkazo methali uliyopewa.
      Muundo
 Kichwa
 methali
yenyewe
Utangulizi
i.        Maana
ya juu/wazi
Maana ya ndani/batini
 Mwili
ü  kisa
kinachofungamana na methali cha kweli au cha kubuni
Þ  Hitimisho
Þ  funzo/maadili
c)   Insha
ya Maelezo
Þ  Inayohusu
kutoa ufafanuzi kuhusu mahali, kitu au jambo fulani kama vile ugonjwa wa
ukimwi, umuhimu wa maji, n.k.
d)   Insha
ya Masimulizi
Þ  Ambapo
unatakiwa kusimulia hadithi, kisa au tukio kuhusu jinsi mambo fulani
yalivyotokea. Huweza kuanzia kwa ‘Ilikuwa…’
e)   Insha
ya Mdokezo
Þ  Ambapo
umepewa mdokezo wa kuanzia (xxx…) au kumalizia (…xxx) k.m. ‘…tangu siku hiyo
alikula yamini kutopuuza ushauri wa wazazi wake tena’
f)    Insha
ya Mjadala
Þ  Ambapo
unatakiwa kujadili suala fulani k.m. ‘Shule za mabweni zina manufaa’ au
‘Kujiajiri ni bora kuliko kuajiriwa’ Jadili.
     Unapaswa:
·  Kuunga
·  Kupinga
·  Kutoa
uamuzi kutegemea upande ulio na hoja nyingi au nzito.
g)   Insha
ya Mawazo
Inayohusu
mambo ya kuwaza kuhusu jambo fulani k.m. ‘MIMI NYUKI’
ü  Ni
nani asiyenifahamu mimi nyuki.
a)   Insha
ya Mazungumzo
 Maongeo
ya kawaida ambayo huandikwa kama tamthilia
  MAZUNGUMZO
BAINA YA…
Muundo
  •  Kichwa
  •  Jina
    la msemaji kwa herufi kubwa likifuatwa na koloni
  •   Maneno
    ya msemaji
  •  maelezo
    ya mandhari na vitendo vya msemaji kwenye mabano
  •  Wazungumzaji
    wasikike kama watu wa kawaida
  •   Pawepo
    na sentensi ndefu na fupi
  •   Matumizi
    ya vihisishi
  •  Ukatizaji
    wa maneno…

2.   TUNGO
ZA KIUAMILIFU
G  Ambazo
hutekeleza kazi maalum na huwa na muundo maalum.
Dayalojia
G  Mazungumzo
kati ya watu wawili au zaidi kuhusu jambo au mada fulani
Þ  DAYALOJIA
BAINA YA…
Þ  Huwa
na utangulizi, mwili na hitimisho
Mahojiano
G  Mazungumzo
yanayoendeshwa kwa muundo wa maswali na majibu
G  (MAHOJIANO
BAINA YA…)
Barua ya Kirafiki
G  Inayoandikwa
kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Muundo
Anwani ya mwandishi (wima au mshazari. Jina
lisiwekwe!)
Tarehe ya kuandikwa barua (22 Februari, 2011)
Mwanzo wa barua (kwa … mpendwa/kwenu…
utangulizi (salamu, kumjuliana hali)
mwili/yaliyomo (ujumbe)
Hitimisho (Kwa leo sina mengi. Wasalimie jamaa
wote. Ni mimi wako/wenu, Jina (wima au mshazari)
Barua Rasmi/Kwa Mhariri
Barua ambazo huandikwa na kutumwa ofisini kwa
kutaka kuomba kazi, kuomba msaada, malalamiko, kutoa maoni gazetini, n.k.
Muundo
ü  Anwani
ya mwandishi (wima au mshazari)
ü  Tarehe
ya kuandikwa (usiweke jina).
ü  Marejeleo
k.m. REJ: SUD/MSS/054/009 (nambari ya kumbukumbu, faili au nambari ya barua)
ü  Cheo
na anwani ya mwandikiwa k.m. Mkurugenzi, Kiwanda cha majani chai cha Kangaita,
S.L.P, 12000, Kerugoya au Mhariri wa Gazeti la ‘Nation’, S.L.P 89000, Nairobi
au KWA ANAYEHUSIKA
ü  Kupitia
kwa: MWALIMU MKUU, anwani
ü  Mtajo
k.m. Kwa Bwana/Bibi/Profesa/Daktari/Mhubiri
ü  Kichwa
cha barua k.m. MINT: OMBI LA KAZI YA UALIMU/MAPENDEKEZO KUHUSU JUMA MRISHO/
MWALIKO WA KUHUDHURIA KONGAMANO LA KISWAHILI
ü  Utangulizi (Mintaarafu
ya tangazo mlilochapisha…naandika kuomba…jinsia…ahadi kufanya kazi kwa bidii)
ü  Mwili
(matatizo, madhara, mapendekezo (naomba, paswa, stahili, naonelea ni bora)
ü  Hitimisho
(Natumai, Nitashukuru…Wako mwaminifu/mtiifu, sahihi, jina /cheo, Chama cha
Kiswahili. Nakala kwa: (i), (ii) (wima au mshazari)
Barua ya Gazetini Iliyohaririwa
ü  Kichwa
(kwa herufi ndogo na usemi halisi)
ü  mtajo
(Mhariri,)
ü  Utangulizi
(Naandika kueleza…)
ü  Mwili
(malalamiko, maoni, maombi, mapendekezo)
ü  Hitimisho
(Natumai…) jina na anwani ya mwandishi)
Tahariri
ü  Maelezo
mafupi ya mhariri wa gazeti kutoa mawazo, maoni au msimamo wa chombo cha habari
anachowakilisha kuhusu suala maalum na muhimu.
      Muundo
GAZETI LA MZALENDO
Februari 24, 2011
HATIMA YA WATAHINIWA
Yaliyomo
Imeandikwa na…
Hotuba
G  Maelezo
yanayotolewa mbele ya watu.
ü  Hutolewa
kwa usemi halisi na huanzia na kuishia kwa alama za usemi.
      Muundo
ü  Anwani
(HOTUBA KUHUSU…)
ü  Utangulizi
(kutaja hadhira kuanzia walio mashuhuri, kuwasalimu, kujitambulisha na
kuwakaribisha na kutambulisha kiini cha hotuba)
ü  Yaliyomo
(kutaja na kufafanua hoja)
ü  Hitimisho
(shukrani na kuwatakia mema katika shughuli zao za kila siku)
Ratiba
G  Mpangilio
wa jinsi shughuli fulani inavyofanyika kulingana na wakati fulani uliotengwa
k.m. sherehe ya arusi, mazishi, siku ya michezo, kutoa zawadi n.k.
      Muundo
ü  Kichwa
(Ratiba ya shughuli gani, ya nani, mahali na tarehe, mgeni wa heshima: …Wageni
mashuhuri: 1….2….3….)
SAA
TUKIO
MHUSIKA
Asubuhi/adhuhuri            
Ku…/watu…
ü  Makaribisho
ü  Maombi
ü  Kutoa
tuzo
ü  Kutoa
shukrani
ü  Kufungwa
kwa maombi
ü  Kuondoka/kufumkana
Shajara
ü  Daftari
ambayo huhifadhiwa matukio yanayofanyika kila siku. Yaweza kuwa ya siku moja,
wiki au mwezi mmoja.
    Aina
a)      Ya
kibinafsi
     JUMANNE 30/8/10
     Leo tulizuru…
b)     Rasmi
(hutumiwa katika ofisi)
     SHAJARA
     JUMANNE MEI 7, 2008
1.              asubuhi
Ku…
2.             
Onyo
Þ  Makatazo.
Tahadhari
Þ  Julisho
kuhusu jambo la hatari.
ONYO!
USISIMAMISHE WALA KUEGESHA GARI
KWENYE ENEO HILI!
TAHADHARI!
DARAJA HILI LINA KASORO
TAFADHALI USILITUMIE
Ilani
Þ  Julisho,
tangazo au notisi.
ILANI
TAFADHALI USITUMIE SIMU
YA MKONO NDANI YA BENKI
ILANI YA SERIKALI KUHUSU KUZUKA KWA UGONJWA WA
KIPINDUPINDU
Serikali imetoa ilani kwa wananchi kuhusu kuzuka
kwa ugonjwa wa kipindupindu. Kila mwananchi anatakikana kuzingatia mambo
yafuatayo ili kudhibiti maambukizi.
a)      Mtu
asinywe maji kabla kuyachemsha
b)      Kupika
chakula hadi kiive vizuri
c)      Kutoenda
haja nje bali kutumia vyoo vya mashimo
d)     Mtu
anawe mikono yake kwa sabuni baada ya kutoka msalani
e)      Mtu
asile matunda au mboga za majani bila kuziosha kwanza
f)       Anayeonyesha
dalili ya ugonjwa wa kipindupindu apelekwe katika kituo cha afya mara moja.
g)      Uchuuzi
wa vyakula umepigwa marufuku
h)      Ufuliaji
nguo motoni pia umepigwa marufuku
Watakaokaidi maagizo katika (g) na (h)
watachukuliwa hatua kali za kisheria ya kutozwa faini ya shilingi elfu tano au
kifungo cha miezi miwili gerezani.
Matangazo
Þ  Majulisho
kuhusu jambo fulani.
a)       Arifa
SHULE YA UPILI YA GATWE
Anwani, tarehe
USAJILI WA …
Sahihi
Jina
Cheo
b)       Kibiashara
Sifa
  •  Lugha
    kwa kifupi
  •   Chuku
  •  Takriri
  •  Alama
    ya (!) na (?)
  •   Michoro
  •  Maonyo
  •  Maelezo
    kukihusu
  •  Kinavyotumika
  •   Ubora
    wake

  Watengenezaji
JINUNULIE UNGA WA MAHINDI WA
JAMBO SIKU YA LEO. UNGA WA JAMBO
UMEONGEZEWA VITAMINI NA MADINI MUHIMU. BEI IMEPUNGUZWA KUTOKA SHILINGI 120
HADI SHILINGI 90. JIPAPIE PAKITI YAKO LEO KABLA BEI HII KUACHA KUTUMIKA


C)Kifo
TANGAZO LA KIFO
Tunasikitika kutangaza kifo cha …Alikuwa…
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi
c)       kazi
SHULE YA UPILI YA GATWE
Anwani, tarehe
NAFASI YA KAZI YA UHASIBU
SIFA ZA MWOMBA KAZI
JINSIA
Awe wa jinsia ya kike.
UMRI
Awe na umri wa miaka isiyopungua25 na isiyozidi 40.
ELIMU
i.        Awe
na shahada ya uhasibu kutoka chuo kikuu au awe na shahada ya diploma ya juu ya
uhasibu
ii.      Awe
amepata alama ya c katika kingereza
KAZI
i.        Kuidhinisha
hati za malipo za shirika
ii.      Kusimamia
shughuli za uhasibu katika idara inayohusika
UZOEVU/TAJRIBA
Awe na uzoevu wa kazi usiopungua miaka 5 kwenye
shirika au taasisi kubwa.
DINI
Awe muumini wa dini ya kikristu na awe ameokoka.
MUDA WA KAZI
Kuanzia saa mbili hadi saa kumi na moja jioni na
masaa mengine ikibidi.
MSHAHARA
Mshahara utategemea elimu ya anayehusika lakini
utakuwa baina ya ksh 24,000 na ksh 45000.
MAELEZO YA ZIADA
i.        Maombi
yote yawe yamewasilishwa kabla ya tarehe 30 mei 2010.
ii.      Maombi
yatumwe kwa:
Katibu,
Halmashauri ya shule ya upili ya Gatwe,
Anwani
iii.    Maombi
yatakayopelekwa baada ya muda wa mwisho hayatajibiwa.
iv.    Maombi
yaandamane na hundi ya shilingi elfu moja ambazo hazitarejeshwa.
Maagizo/Maelekezo
ü  Maelezo
kuhusu namna ya kufika mahali kutoka kituo fulani au maelezo kuhusu njia ya
kutumia kitu au huduma fulani.
Sifa
a)      Maelezo
wazi
b)      Michoro
au ramani
c)      Dira
d)      Huhusika
maonyo
e)      Tarakimu
k.m. 1×3
f)       Matumizi
ya herufi nzito.
Mifano
a)      Maagizo
ya daktari kwa mgonjwa wa kisukari.
b)      Maelekezo
ya kutoka nyumbani hadi shuleni mwenu.
c)      Jinsi
ya kutumia dawa za wadudu
Kujaza Fomu
G  Karatasi
ambayo ina nafasi ya kuandika maelezo ambayo yanatakiwa.
a)      Soma
fomu kwa makini kabla ya kujaza chochote.
b)      Andika
maelezo kwa muhtasari.
c)      Usijaze
kama huna hakika kwenye sehemu Fulani.
d)     Usifutafute.
e)      Itumie
alama inayostahili wakati wa kujaza fomu.
MAELEZO YA KIBINAFSI
TAREHE……………………………………………………
JINA………………………………………………………………
JINSIA…………………………………………………………………
UMRI…………………………………………………………
TAREHE YA KUZALIWA…………………………………………
URAIA………………………………………………
NAMBARI YA KITAMBULISHO………………………………
KAZI……………………………………………………
MKOA…………………………………………………………………
WILAYA……………………………………………………………
SIMU………………………………………………………………
SAHIHI………………………………………………………
TAREHE………………………………………………………..
Hojaji
  Maswali
ambayo hutumiwa kama msingi wa kufanyia utafiti na huelekezwa kwa mhojiwa.
Aina
a)       Hojaji
Wazi
  Hojaji
yenye maswali ambayo mhojiwa anaruhusiwa kuyajibu kwa maneno yake mwenyewe.
UCHAGUZI NA VIONGOZI
1.      Una
maoni gani kuhusu uchaguzi wa kila baada ya miaka mitatu?
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
2.      Kwa
nini una maoni hayo?
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
3.      Wewe
ungependelea utaratibu gani wa uchaguzi?
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
4.      Je
ni kweli viongozi hung’ang’ania mamlaka?
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
5.      Je
viongozi hung’ang’ania uongozi kwa sababu zipi?
a)      …………………………………………………………….………………………
b)      ……………………………………………………………………………………
c)      ……………………………………………….….…………………………….….
b)       Hojaji
Funge
ü  Hojaji
ambapo mhojiwa anapewa majibu kadha ambayo anatakiwa kuchagua mojawapo bila
kuwa na uhuru wa kuandika atakayo.
MATATIZO YA KIJAMII
Tia alama kwenye jibu unaloafiki
a)      Jamii
yetu inawakandamiza wanawake?
Ndiyo
(    )   La (    )
b)      Tatizo
kubwa la jamii yetu kwa sasa ni umaskini na ugonjwa.
Kweli
(     )  Si kweli
(     )
Mialiko
 Barua
ambayo hupeleka taarifa kwa mtu kumuomba ahudhurie sherehe fulani.
a)       Rasmi
(kadi au barua rasmi)
Muundo
  •  Jina
    la mwalikaji/waalikaji (Bwana/mabwana/bibi/kasisi/daktari
  •   Jina
    la mwalikwa
  •  Sherehe
    (ndoa, mchango wa pesa, Kuna aina mbili za mialiko.
  •   Kusherehekea/kuadhimisha…)
  •  Kuhusu
    nani
  •   Mahali
    pa kukutanika
  •   Tarehe
  •   Wakati

  Anwani
na nambari ya simu ya mwalikaji ambapo jibu litapelekwa kushoto chini (Majibu
kwa…wima)
b)   Kirafiki
(barua ya kirafiki)
 Sehemu
ya mwili itoe habari zote muhimu katika mwaliko.
Risala
 Taarifa
inayotoka kwa mtu au watu inayoeleza haja fulani k.m. risaala ya rambirambi,
risala ya heri njema, ya waajiriwa kwa mwajiri au kinyume.
RISALA YA RAMBIRAMBI/HERI NJEMA KWA…KUFUATIA
Mimi wako…
Resipe
Jumla
ya hatua na kanuni ambazo hufuatiwa na mtu anayenuia kupika au kuandaa kitu
fulani.
UPISHI WA PILAU
Walengwa/walaji
     Mipakuo mine (kwa
watu wanne)
Viambata
a)      Vikombe
viwili vya mchele
b)      Gramu
25 za mafuta ya majimaji
c)      Vijiko
viwili vidogo vya pilau masala
d)     Nusu
kilo ya nyama
e)      Vitunguu
vinne vya ukubwa wa wastani
f)       Vikombe
vinne vwa maji
Hatua za Upishi
a)      Kaanga
vitunguu katika mafuta hadi rangi yake ikaribie rangi ya udhurungi
b)      Chemsha
nyama pekee hadi ilainike
c)      Ongeza
nyama kwenye sufuria yenye vitunguu na upike kwa dakika tano
d)     Ongeza
mchele na uchanganye kwa mwiko
e)      Ongeza
maji na uache mchanganyiko utokote kwa dakika kumi na tano
f)       Pakua
pilau ikiwa tayari
Orodha Ya Mambo
Mlolongo
wa vitu vilivyoandikwa.
MAHITAJI MUHIMU YA KURUDI SHULENI TAREHE 5/1/2010
a)      Sukari
kilo mbili
b)      Dawa
ya meno ya gramu hamsini
c)      Koko
gramu 500
d)     Sabuni
sita za kipande
e)      Kalamu
nne za rangi
f)       Penseli
moja
g)      Rangi
ya viatu ya gramu 40
Tahakiki
Maandishi
ya kuchambua maandishi ya fasihi.
USASA WAKUTANA NA UKALE
Anwani: Kitumbua Kimeingia Mchanga
Mwandishi: Said A. Mohamed
Mchapishaji: Oxford University Press
Mhakiki: Amina Fuzo
Maudhui
Meme
Barua
ambazo huhusisha matumizi ya ya vifaa vya umeme kama talakilishi,
kiepesi/nukulishi/faksi au simu ya mkonono/tamba/rukono.
Barua za Mdahilisi/Pepe
Ambazo
hutumwa kwa tarakilishi kwa njia ya mtandao.
Ijumaa Machi 30, 2007 saa 08:09:19
Kwa: ahmed@african online.ke
Nakala kwa: amina @ mwananchi.com
MINT/KUH:
Barua ya kawaida
Hitimisho: Aisha Kizito Makwere
Memo
Taarifa
fupi ambayo huandikwa ofisini kuhusu mambo ya ndani kutoa maelekezo, maelezo au
kukumbusha kuhusu jambo fulani. Ujumbe huwa mfupi na huhusu suala moja tu.
SHULE YA UPILI YA GATWE
Anwani
MEMO
REJ: km/01/06
KUTOKA: Mwalimu Mkuu
KWA: wafanyakazi wote
MADA: likizo fupi
TAREHE: 28/2/2011
Ujumbe
Sahihi
Jina
Cheo (mwalimu mkuu)
Taarifa
Kuarifu
kuhusu habari mpya
UCHOCHEZI
Hitimisho
Mariga Mununga
Mwanahabari
Wasifu
Maelezo
ya mtu kuhusu mtu mwingine tangu kuzaliwa mpaka alipo au kufa kwake.
WASUFU WA NDUGU YANGU JUMA
Tawasifu
Maelezo
ya mtu kujihusu
TAWASIFU YANGU
Vidokezo
  •  Jina
    lake/lako
  •   Jinsia
  •   Anakotoka
  •   Umri
  •   Kuzaliwa
  •   Maumbile
  •   Elimu
  •   Kazi
  •   Hadhi
    ya ndoa
  •   Lugha
  •   Lakabu
    na sababu
  •   Umaarufu
  •   Uraibu 
  • Wasifutaala/Wasifu Kazi

G  Maelezo
rasmi kuhusu mtu binafsi ambayo huambatanishwa na barua ya kuomba kazi.
WASIFUTAALA WANGU
MAELEZO BINAFSI
Jina                                   : Farida
Almasi Juma
Tarehe ya
Kuzaliwa           : 7-6-1980
Umri                                  : miaka
22
Mahali pa
kuzaliwa            : Voi
Jinsia                                : mwanamke
Hadhi ya
ndoa                   :
Nimeolewa/kapera
Nambari ya kitambulisho  : 12345678
Uraia                                 :
Mkenya
Lugha                                :
Kiswahili, Kingereza, Kikuyu
Anwani ya
kudumu           :
S.L.P. 1600, Voi
Barua pepe                        :
Farial@yahoo.com
Simu
tamba                       :
9876543210
ELIMU
1.1.     Chuo
Kikuu cha Maseno (Shahada ya Uhasibu)
1.1.   Shule
ya upili ya Shimoni (Shahada ya KCSE)
1978-1987   Shule
ya Msingi ya Umazi (shahada ya KCPE)
TAJRIBA
Mpaka
sasa    Mhasibu
katika shule chekechea ya Mtakatifu Yohana
HABARI ZA ZIADA
URAIBU
a)       Kusoma
vitabu vya sarufi na fasihi
b)       Kutembelea
wajane, mayatima na wagonjwa
c)       Kuandika
mashairi
AZIMIO LANGU
a)       Kupaa
kitaaluma kwa kuendeleza masomo yangu hadi kiwango cha uzamifu
b)       Kuwa
mhasibu bora zaidi nchini kwa matendo na kuwapa wananchi huduma za kufaa
WAREJELEWA
1.           Profesa
Hassan Muoso,
       Chuo
Kikuu Kenyatta,
       S.L.P.43844,
       Nairobi.
2.       Maimuna
Njavu Mukota,
      Shule ya Upili
ya Alliance,
      S.L.P. 1 234,
      Nairobi.
Kumbukumbu
G  Maelezo
kuhusu yaliyojadiliwa na kuafikiwa katika mkutano.
Muundo
Kichwa (kumbukumbu za mkutano wa kamati/jopo gani,
uliofanyika wapi, tarehe gani, saa ngapi hadi gani na majira)
Waliohudhuria (mwenyekiti, katibu, mweka hazina,
wanakamati)
Waliotuma udhuru kwa kutohudhuria
Waliokosa kutuma udhuru wa kutohudhuria
waalikwa
Ajenda
a)      Kufunguliwa
kwa mkutano (KUMB 3/2OO9)
  Kufunguliwa
kwa mkutano, mwenyekiti kuwakaribisha na kuwashukuru waliohudhuruia na kumwomba
… aongoze kwa maombi.
b)      Kusoma
na kudhibitisha kumbukumbu za mkutano uliotangulia
  Kusomwa
na katibu, aliyependekeza na aliyedhibitisha.
c)      Masuala
yaliyotokana na kumbukumbu hizo
 (a)
KUMB 8/2008 ununuzi wa miti
d)     Shughuli
nyinginezo
e)      Kufunga
mkutano (KUMB 7/2009)
  Mkutano
uliisha saa ngapi, maombi yaliongozwa na nani, na mwingine ukapangwa kuwa wa
siku gani.
Maneo kama walikubaliana, waliafikiana,
alipendekezwa, ilisemekana, waliambiwa, ilionelewa ni bora, walishauriwa,
ilidaiwa, aliomba, n.k.
THIBITISHO
KATIBU                        TAREHE……………
SAHIHI ……………
MWENYEKITI             TAREHE
……………. SAHIHI ……………
Ripoti
 Maelezo
kuhusu mtu, kitu au tukio
a)       Ripoti
ya Kawaida
  Swali
huanzia kwa ‘Wewe kama katibu wa chama…’
Muundo
  1.   Kichwa
    (ripoti ya kamati/jopo gani)
  2.   Utangulizi
    (maelezo mafupi ya jumla kuhusu chama)
  3.   Shughuli
    za chama (i, ii, iii)
  4.   Hitimisho
    (matumaini, mwito kwa wengine wajiunge, wajitahidi)
  5.   Ripoti
    imeandikwa na (jina, cheo/katibu, sahihi, tarehe)

b)       Ripoti
Maalum
  •  Kichwa
    (ripoti ya jopo la kutathmini usalama barabarani)
  •   Utangulizi/Hadidu
    za rejea (ripoti ilihitajika na kamati gani, uchunguzi ulifanywa kubainisha
    nini, matokeo kuelezewa chini pamoja na mapendekezo kutolewa)
  •   Jopo
    (majina na vyeo vya wanajopo waliohusika)
  •   Utaratibu/
    hatua za utafiti (wanakamati walifanya nini (kamati iliwahoji…ilifanya ukaguzi
    wa magari, iliwapa baadhi ya wasafiri hojaji wakajaza, ilipiga picha za video,
    mashauriano)

  •  Matokeo
    (kamati iligundua kuwa: (a)
  •  Mapendekezo
    (suluhisho la shida)
  •  Hitimisho
    (ripoti imeandikwa na, sahihi, jina, cheo/katibu, tarehe 21 Machi 2011.

3.   UTUNGAJI
WA/INSHA ZA KISANII
a)      michezo
ya kuigiza
b)      hadithi
fupi
c)      mashairi
d)     mafumbo
e)      vitanza
ndimi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *