TAHAKIKI YA UMBILE

Mwanamke

mwanamke,mwanamke na simba,mwanamke na nguvu,nguvu ya mwanamke,mwanamke ngangari,ameoa mwanamke mwenzake,dereva mwanamke wa lori la mafuta,swahili fairy tales,kenya,mange,mwakasege,mke,global tv online,mme,matatizo ya wanawake,wanawake duniani,semina ya wanawake 2020,magufuli,semina ya wanawake 2019,mwakasege 2019,mwisho wa dunia,wanajiuza,make money,kukomoana,masomo mwakasege,mwakasege vijana,dawa ya,wasafi,malaya
  1. Alikuwa mwanamke wa elfu. Hakika, Mungu alikuwa amempoteza hurulaini wake peponi.
  2. Meno ya bisi/mchele yaliyopangwa yakapangika kinywani kama lulu katika chaza/bao katika vidu/kete.
  3. Mwanya wa haiba na mvuto /mwanya wa mwangaji.
  4. Midomo ya miteko na kasiba.
  5. Vidu vilivyoshobweka barabara mashavuni.
  6. Urembo wa sahani.
  7. Macho ya chawa kama Mchina au Maninga ya gololi/kikombe
  8. Pua ya mtepeto kama Mhabeshi au pua ya kitara.
  9. Shingo ya upanga
  10. Masikio ya mchanuko
  11. Mikono ya mbinu
  12. Kope zake zilichanwa zikachanika kwa uzuri wa kupendeza na kutamanika.
  13. Kiuno chake kilichezacheza kwa migwayo ya kumezea na kutamanika.
  14. Mabega ya mfumbati
  15. Nywele za julfa zilizofungwa kwa mafundo ya kupendeza na kutaanisi.
  16. Kiuno cha bunzi au kiuno cha nyigu.
  17. Miguu ya cherehani bila matege wala mang’ombo/ matege wala maguta
  18. Alikuwa mfua uji mwenye umbo la shani.
  19. Aliumbwa akaumbika ungalifikiri Dayani alichukua siku ayami kumwumba.
  20. Mwingi wa tabasamu.
  21. Uso wa haiba au uso wa kifuu cha nazi au wajihi wagivu/uso wa nuru.
  22. Nyusi za mwezi mwandamo/mwezi kongo.
  23. Kifuani dodo zake (viduta vyake) hazikuachwa nyuma zilisimama imara kama vitumbua viwili vililvyochongwa na mfinyanzi stadi/gwiji/galacha na kutiwa hamira.
  24. Umbo la wastani
  25. Kiuno chake kilikuwa sawa na namna yai lilivyo katikati.
  26. Uzuri wake usingeelezwa kwa maneno matupu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *