NAOGOPA.
Uko wapi mama Boi,kunyesha bado kungali
Nonavyo sitoboi,niletee muwavuli
Wandamane na kikoi,baridi shadidi kali
Ikiwa mwanga umekosa,nawe tumia akili.
Niendapo sitafika,nimeola giza kuu
Mvua inamwaika,yatateleza maguu
Chinile nitaanguka,ninuwe miguu yuu
Njoo hapa mwanga wangu,’tumiye hino akili
Muhibu fanya haraka,natapia kwenda too
Tumboni naangaika,naomba haraka ndoo
Mapema usipofika,hapa nitashika moo
Kwa kutii fanya hara,matumbo yakorogana.
Hongera