ULEMAVU
Kilema/Uatilifu –ni kasoro iliyoko kwenye kiungo au viungo vya
mwili.
Mlemavu – ni mtu au mnyama mwenye kasoro ya kiungo au viungo.
A)Hali ya ulemavu
- Mafungamavi -Miguu iliyopindika kwa ndani.
- Kidazi -Ukosefu wa nywele kichwani.Pia upara.
- Kigutu -Kiungo cha mwili kilichokatika.
- Upara-Hali ya kutokuwa na nywele kichwani.
- Mangombo -Miguu iliyobinukia mbele.
- Matege -Miguu iliyopindika kwa nje na kuacha nafasi kati ya mguu mmoja na mwingine.Pia gobwe au magombi
- Magutao -Miguu iliyobinukia nyuma.
- Pacha-Kwenda kama mwenye kilema cha miguu.Pia Chechemea au dengua.
- Kinyonyoke -Mtu asiyemea nywele kichwani na zikimea hukatika.
- Kinyenyezi -hali ya kutoona vizuri.
B)Walemavu mbalimbali
- Kipofu -Mtu asiyeweza kuona kabisa.
- Chongo -Mtu aliye na jicho moja lililoharibika.
- Njorinjori -mtu mwenye miguu mirefu kupita kiasi.
- Kiguu-mtu ambaye mguu wake mmoja una kilema aghalabu kupindika.Pia kiguru.
- Kibyongo-mtu mwenye nundu mgongoni.Pia kigongo, kiduva au kijongo.
- Kisaka -mtu mwenye kimo kifupi.Pia kibirikizi au kidurango.
- Chakaramu -mtu aliye na kichaa.Pia afkani.
- Chotara -mtu aliyezaliwa na wazazi wa rangi tofauti au mbalimbali.Pia shombe au suriama.
- Mziavu-mtu aliyevia akili.
- Buge -mtu aliyekatika kidole au asiye na kidole cha mkono
- Kikono -mtu mwenye kilema cha mkono.
- Mpapachi -mtu aliye na meno yaliyopandana.
- Toinyo -mtu aliyekatika pua.
- Kigutu –kiungo cha mwili kilichokatika.
- Kipara-Mtu asiye na nywele kichwani.
- Makengeza -mtu aliye na mboni zisizo katikati bali upandeupande. Pia mawenge.
- Mbedu -chongo aliye kengeza.
- Bubu -mtu asiyeweza kusema kabisa.
- Kigugumizi-nmtu anayesita katika kusema au kusoma Pia kitata.
- Kithembe -mtu anayetamka aneno kivyake kwa ncha ya ulimi,
- Kiziwi-mtu asiyeweza kusikia.Pia kiduko,
- Masito –mtu asiyesikia vizuri lakini si kiziwi.
- Kibwiko -mtu mwenye vidole vilemavu.
- Kigego -mtu anayezaliwa akiwa tayari na meno au mtoto ambaye meno ya juu yametangulia ya chini
- Kibogoyo-mtu asiye na meno au mwenye meno machache. Pia mhangi.
- Kibunye-mtu aliyekatika sikio au masikio yote.
- Kiwete -mtu aliyelemaa miguu yote.
- Buda-mwanamume mzee sana aghalabu asiye na meno.