VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE

 VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE 
news,kihaya,swahili introductions,learn kiswahili,akili na mimi,ubongo kids,mama ndege,ekihaya,hadithi,kujitambulisha,sauti,ebikoikyo,emigani,bwenge,uf,masikini punda,learn swahili,nyimbo za kiswahili,poor donkey kids song in swahili,kreative generation,churchill show,dan ndambuki,mwalimchurchilu kingangi,comedy drama,funny,kids festival,sande yesu,nyimbo za watoto,daily nation breaking news,africa,business,sports,blogs,photos

Adui lakini po pote uendako yuko nawe-Inzi
Afahamu kuchora lakini hajui achoracho- Konokono
Aliwa, yuala; ala, aliwa-Papa
Ajenga ingawa hana mikono- Ndege
Ajifungua na kujifunika-Mwavuli
Akitokea watu wote humwona-Jua
Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni-Ugonjwa
Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza- Mgomba
Alipita mtu ana bunda la mshale-Mkindu
Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo- Inzi
Afuma hana mshale-Nungunungu
Amchukuapo hamrudishi-Kaburi
Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi- Giza
Amefunua jicho jekundu-Jua
Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri- Mbegu
Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe-Koa/ Konokono
Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote- Mgomba
Amekula ncha mbili- Wali
Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe- Kaburi
Anakuangalia tu wala halali au kutembea- Picha
Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba-Mchanga
Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele-Ardhi
Anakula lakini hashibi- Mauti
Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana- Moto
Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’- Kitanda
Ashona mikeka wala hailali-Maboga
Askari wangu wote wamevaa kofia upande- Majani
Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi –Chunguchungu
Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili-Fedha
Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti-Mvua
Atolewapo nje hufa-Samaki


B



Babu amefunga ushanga shingoni-Mtama/Nazi
Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe- Muwa
Babu hupiga kelele akojoapo- Mvua
Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo- Mti na shoka
Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani- Mlango
Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi? –Siafu
Bak bandika, bak bandua.-Nyayo
Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali-Muwa
Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea- Sisimizi
Babako akojoapo hunung’unika- Mawingu
Bibi kikongwe apepesa ufuta- Kope za macho
Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroki –Kinu cha kutwangia





C

Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana- Dunia na mbingu
Chang’aa chapendeza, lakini hakifikiwi- Jua
Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja- Mwezi/Jua
Chakula kikuu cha motto- Usingizi
Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani- Nyama na mfupa

Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo- Pazia
Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka-Mjusi/Panya
Cheupe chavunjika manjano yatokea- Yai




D

Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe-Jani likwanyukapo
Dada yangu kaoga nusu- Jiwe mtoni
Drrrrrh1 Ng’ambo-Daraja la buibui

Dume wangu amelilia machungani- Radi

F

Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani.-Mwezi na nyota angani
Fika umwone umpendaye- Kioo
Fuko kajifukia, mkia kaacha nje- Kata mtungini
Funga mizigo twende Kongo- Mikia ya mbwa

H


Hachelewi wala hakosei safari zake- Jua
Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo- Maji
Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea- Nywele
Hakionekani wala hakishikiki- Hewa
Hakisimami, na kikisimama msiba- Moyo
Hakuchi wala hakuchwi- Kula
Halemewi wala hachoki kubeba- Ardhi
Hamwogopi mtu yeyote- Njaa
Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua- Ukucha
Haoni kinyaa- Mvua
Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu- Mvua
Hasemi, na akisema hatasahaulika-Kalamu
Hasimamishwi akiwa na ghadhabu- Upepo
Hata inyeshe namna gani haifiki humu-Kwapani
Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto- Pua ya mbwa
Hata Mzungu ameshindwa-
Mauti 
Hauchagui chifu wala jumbe- Utelezi
Hausimiki hausimami-Mkufu
Hawa wanaingia hawa wanatoka- Nyuki mzingani
Hesabu haihesabiki- Nyota
Huitumia kila siku lakini haiishi- Miguu
Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu- Jua
Huku unasikia ‘pa’ Huku unasikia ‘pa! –Mkia wa kondoo
Hula lakini hashibi- Sindano
Hulala tulalapo, huamka tuamkapo-Jua
Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue-Matendegu ya kitanda
Huna macho lakini wakamata wanyama- Ndoana
Hupanda mtini na mwenye kichaa wake- Kivuli
Hutembea watatu- Mafiga
Hutoka upesi sana lakini hasalimu- Kuku
Huwafanya watu wote walie- Moshi
Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi-Chungu jikoni
Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi- Mbegu na matunda



I
Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali– Kifo
Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka- Herufi “K”

J
Jiwe litoalo maji- Macho
Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako? -Nywele kichwani
Jembe la Wangoni haliishi- Miguu/Nyayo

K
Kaburi la mfalme lina milango miwili- Kata ya kuchukulia Maji kichwani
Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote- Kizingiti cha mlango
Kama unapenda, mbona usile? –Ulimi
Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa   nikautumia- Nazi

Kilimsimamisha chifu njiani- Chawa
Kina mikono na uso lakini hakina uhai- Saa

Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi-Chongo
Kunguru akilia hulilia mirambo- Mtoto akililia maziwa
Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza kupata miwili- Watoto wa ng’ombe na mbuzi
Kwetu mishale na kwenu mishale- Mikia ya panya
Kwetu twalala tumesimama- Nguzo za nyumba
Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege- Nyoka au samaki
Kuku wangu amezalia miibani-Nanasi au chungwa
Kuku wetu hutagia mayai mikiani- Matunda
Kuna mlima mmoja usio pandika-Nafasi kati mdomo na pua
Kinaniita lakini sikioni- Mwangwi
Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji- Taa ya utambi
Kisima kidogo kimejaa changarawe- Kinywa na meno
Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi- Mimba
Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu- Moto

Kapanda mti pamoja na uchawi wake- Tumbaku inaponuswa puani
Kidimbwi kimezungukwa na majani- Macho
Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa- Maziwa
Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele-Mvua
Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma- Paka na mkia wake
Kila mtu atapitia malango huo- Kifo
Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita- Mlango

Kitu changu asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu mitatu- Maisha ya binadamu
Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu- Kipara
Kombe ya Sultani Ii wazi- Kisima
Kondoo wangu amezaa kwa paja- Mhindi
Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima- Konokono

Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni- Jua
Kileee! Hiki hapa- Kivuli
Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe- Kuku aatamiapo mayai
Kiti nyikani- Uyoga
Kondoo za mtoto zamaliza mavuno- Jiwe la kusagia
Kufanya kwa ridhaa mojamoja- Kusuka mkeka

Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje- Ghala

L
Likienda hulia, likirudi halilii- Debe aka buyu
Likitoka halirudi- Neno
La mgambo limelia wakatoka weusi tu- Chunguchungu
Liwali amekonda lakini hana mgaga- Sindano

M
Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini- Mwaka
Mtoto asemea pangoni- Ulimi mdomoni

Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi- Mvua
Mzee Kombe akilia watu hufurahi- Mvua
Mzizi wa miti hutokea mbali- Siafu
Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje-Hindi
Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri- Nyuki
Mwanang’ang’a hulia mwituni- Shoka
Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote- Tufani
Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano- Mawazo
Mvua hema na jua hema- Kobe
Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme- Nafasi kati ya mdomo na pua ya ngombe
Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe- Buibui na utando wake
Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki- Mkungu wa ndizi
Msitu ambao haulii hondohondo- Mimba

Mama ametengeneza chakula lakini hakula- Chungu cha kupikia
Mbona kinakumeza lakini hakikuli? –Nyumba
Mfalme hushuka kwa kelele- Mvua
Mfalme katikati lakini watumishi pembeni- Moto na mafiga
Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote kwanza- Hindi
Mhuni wa ulimwengu- Inzi
Mkanda mrefu wafka mpaka pwani- Njia
Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi- Hindi
Mlango wa nyumba yangu uko juu- Shimo la mchwa
Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu- Sima/Ugali
Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana? -Mafiga
Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani? –Katani
Mchana ‘ti’ usiku ‘ti’- Mlango
Mdogo lakini humaliza gogo- Mchwa
Mfalme amesimika mkuki wake hapa name 
nikausimika wangu kando yake, baadayehatukuitambulisha tena- Kohozi
Mlimani sipandi- Maji
Mlima umezuia kutazama kwa mjomba- Kisogo
Mlima wa kupanda kwa mikono- Mlima
Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!- Ngoma na upatu
Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu- Kichwa na masikio
Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa- Jiwe
Mwadhani naenda lakini siendi- Jua
Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea- Kinyesi na inzi
Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani- Kunguru

Mwezi wangu umepasuka- Kweme

N

Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia- Utomvu
Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani- Nzige
Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu- Sauti ya nziga
Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa- Kivuli
Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa- Mgomba
Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja- Kuangua tunda ama nazi
Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki-Mtego
Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu- Maisha
Nina kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi- Jina
Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua- Dada
Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana siwezi kumwazima- Mke

Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu- Kichwa
Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu- Jua au mwezi
Njia yapitwa siku zote lakini haina alama- Njia ya jua au mwezi
Njoo hapa nije hapo- Kiraka
Nne nne mpaka pwani- Matendegu
Nusu mfu nusu hai- Sungura alalapo
Nyama ya Reale haijai kikombe- Mkufu
Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo-Kitanda
Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja- Mwembe
Nyumba yangu ina milango mingi- Kichuguu
Nina mwezi ndani ya bakuli- Maziwa
Nina ng’ombe wangu nisipomshika mkia hali majani-Jembe
Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa- Mdomo
Nina pango langu lilojaa mawe- Kinywa
Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe- Kunguru
Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki- Mafiga
Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi-Kivuli
Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi- Jiwe
Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi- Maji na mkojo
Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi- Chungu cha kupikia
Ninakwenda naye na kurudi naye- Kivuli
Nyumba yangu ina nguzo moja- Uyoga
Nyumba yangu kubwa, haina mlango- Yai
Nyumba yangu kubwa, haina taa- Kaburi
Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni- Konokono
Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia- Mwiba
Nakikimbilia lakini sikikuti- Njia
Nakupa lakini mbona huachi kudai- Tumbo
Nameza lakini sishibi- Mate
Namkimbiza lakini simkuti- Kivuli
Namlalia lakini halii- Kitanda
Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa- Kigino
Nanywa supu na nyama naitupa-Muwa
Napigwa na mvua na nyumba ipo- Matunda ya pua/Kwapa
Natembea juu ya miiba lakini hainichomi- Miiba
Natembea juu ya miiba lakini sichomwi– Ulimi
Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni- Mbwa
Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana- Mzinga wa nyuki kwa nje
Natengeneza mbono lakini alama hazionekani- Mzinga wa nyuki
Ndege wengi baharini- Nyota
Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani- Macho
Ngoja nikumbuke- Boga changa
Ng’ombe wa baba watelemka mtoni- Mawe mtoni
Ng’ombe wa babu huchezea miambani- Mijusi
Ng’ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii- Vibuyu
Ng’ombe za babu zinalala na mkia nje-Viazi vitamu udongoni
Ng’ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu- Pesa/Nyayo
Ng’ombe wangu ni weupe kwatoni- Katani
Ng’ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja- Fimbo ya kuchunga
Ngozi ndani nyama juu- Firigisi
Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa- Nyusi
Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna- Kioo
Nikienda arudi, nikirudi aenda- Kivuli majini
Niiita ‘baba’ huitika ‘baba’- Mwangwi
Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki- Popo
Nikimpiga huyu huyu alia- Utomvu wa papai
Nikimpiga mambusu- Puliza kidole wakati unapojikwaa
Nikimwita hunijibu nani- Mwangwi
Nikipewa chakula nala bali natema- Shoka
Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya- Majani makavu na mabichi
Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo- Kivuli
Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza?- Shimo
Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali- Jicho
Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia- Umande na jua
Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha ezekwa majani- Mahindi machanga
Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja- Jani la mgomba la nchani
Nilimkata alafu nikamridhia- Kupanda mbegu
Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi- Fuko

Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto- Kivuli
Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku
           kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi
           walikwenda Rumi? Hakuna
Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi- Ulimi kinywani
Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho- Chura
Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani- Kivuli
Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu- Njia
Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu- Masikio
Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani- Moto
Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng’ombe mkia- Kata
Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani- Mimba
Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni- Nyota
Nimezaliwa na mguu mmoja- Uyoga
Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi- Ulimi na meno

Nilipandia majanini nikashukia majanini- Mwiba
Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni-Manyigu
Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana- Kiazi kikuu
Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati- Pelele
Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka- Mzinga wa nyuki
Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia- Mjusi

O

Ondoka nikae- Maji ya mfereji

P
Paa alipenga hata pua ikapasuka- Mbarika
Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona; wa pili aliyaona maji lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka.
Ni nani hawa?- Wa kwanza ni Mtoto tumboni mwa mamake, wa pili ni Mtoto aliyebebwa mgongoni, wa tatu ni mama mwenyewe
Panda ngazi polepole- Sima ya ugali
Para hata Maka- Utelezi
Pete ya mfalme ina tundu katikati- Kata ya kuchukulia mizigo
Poopoo mbili zavuka mto-Macho
Po pote niendako anifuata- Kivuli

R
Reli yangu hutandika ardhini- Siafu
Rafiki yangu ana mguu mmoja- Uyoga
Ruka Riba- Maiti

S

Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja- Nywele kichwani

Sijui afanyavyo- Nyoka apandavyo mtini
Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu.Ni nani huyo?- Mtoto wangu
Shamba langu miti mitano tu- Mkono wa vidole
Subiri kidogo!- Miiba
Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa- Maji

Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo- Njia
Sijui aendako wala atokako- Upepo

T

Tega nikutegue- Mwiba
Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke-Mahindi ama yai
Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania- Mbono
Tumvike mwanamke huyu nguo- Kuezeka nyumba
Tunajengajenga matiti juu- Mapapai
Twamsikia lakini hatumwoni- Sauti
Taa ya bure- Jua au mwezi
Taa ya Mwarabu inapepea- Kilemba
Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa- Makamasi

Tonge la ugali lanifikisha pwani- Jicho
Tukate kwa visu ambacho hakitakatika- Maji
Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu- Kucha
Tuliua ng’ombe na babu, kila ajaye hukata- Kinoo
Tuliua ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa- Mbingu na nchi
Tandika kitanga tule kunazi- Nyota
Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia- Mkufu
Tatarata mpaka ng’ambo ya mto- Utando wa baibui
Tatu tatu mpaka pwani- Mafiga

U

Ukoo wa liwali hauna haya- Wanyama
Ule usile mamoja- Kifo
Umempiga sungura akatoa unga- Funda la mbuyu
Unatembea naye wote umjiao atakuona- Bakora
Upande wote umjiao atakuona- Kinyonga
Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba- Mwangwi
Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia- Fisi
Ukimwona anakuona- Jua
Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu- Nywele
Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto- Kinyonga
Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo- Mwamba
Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki- Moshi
Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini- Tundu la sindano

V

Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki- Moto

W

Wake wa mjomba kimo kimoja- Vipande vya kweme
Wako karibu lakini hawasalimiani- Nyumba ama kuta zinazoelekeana
Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja- Matone ya mvua
Wanameza watu jua linapokuchwa- Nyumba
Wanamwua nyoka- Watu wanaotwanga

Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu- Fuu
Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu-Jogoo
Wanastarehe darini- Panya
Wanatembea lakini hawatembelewi- Macho
Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka- Maboga
Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani- Viroboto
Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu
           haonekani tena- Kivuli
Watoto wangu wote wamebeba vifurushi-Vitovu
Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao?- Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo
Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu- Kuku, katani au mahindi

Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana- Mlango
Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu-Nyota
Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe- Vipepeo

Watu wote ketini tumfinye mchawi- Kula ugali
Wewe kipofu unaenda wapi huko juu?- Mkweme

Y
Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo- Njia

Z

Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu- Moto
Ziwa dogo linarusha mchanga- Chungu jikoni
Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana- Kingo za mto







we hope this article helped you to know about Proverbs.You may also want to see href =”” target =”_blank>

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *