Uakifishaji

Uakifishaji
Neno uakifishaji linatokana na kitenzi ‘akifisha’ chenye maana ya kutumia alama za lugha ifaavyo katika
maandishi. Sarufi ya lugha yoyote ile hutegemea uakifishaji ufaao.
Kikomo (.)
 Kikomo pia huitwa nukta, kituo au kitone. Matumizi yake ni :
(a) Kuonyesha mwisho wa sentensi.
Mifano:
1. Kababy ameenda ughaibuni.

(b) Katika uandishi wa tarehe ili kutenga siku, mwezi na mwaka.
Mifano:
1. Korona ilichipuka  tarehe 31.12.2019
(c) Kuandika ufupisho wa maneno.
S.L.P- Sanduku La Posta
Bw.-Bwana
Bi. – Bibi
Mf. – Mfano
(d) Kutenga senti katika pesa.
1. Shilingi 20.50- Shilingi ishirini na senti hamsini.
2. Shilingi 100.30 – Shilingi mia moja na senti thelathini.
(e) Katika uandishi wa nambari kuonyesha sehemu isiyo nzima.
2. Tani 100.5- Tani mia moja nukta tano.
(f) Katika uandishi wa saa ili kutenga saa na dakika,
1. Saa 5.30 jioni – Saa kumi na moja unusu jioni.
Koma (,)

Koma pia huitwa mkato au alama ya mpumuo. Koma hutumiwa:
(a) Kutenga orodha ya vitu zaidi ya viwili. Mifano:
1. Nimenunua nyanya, dania, sukuma na mayai.
2.Simba, ndovu, nyati, kifaru na chui ni wanyama hatari. 
(b) Katika uandishi wa anwani 
Mfano: Shule ya upili ya lling’arooj,
S.L.P 23001,
Kajiado
(c) Kuonyesha utengano wa kimawazo katika sentensi.
Mifano:
1. Wewe nenda, mvua ikinyesha utanunua mwavuli.
(d) Kuandika tarakimu. Mfano:
1. 50,000
2. 371,000
3. 2,720,000
(e) Katika sentensi ndefu ili kuonyesha mapumziko.
1. Niliteremka na barabara hiyo na nilipofika pale ilipopinda,mvua ilianza kunyesha ghafla.
Alama ya kiulizi (? )
Hutumika kuulizia swali. Alama hii huwekwa mwishoni
mwa sentensi.
1. Kigoda cha Mstahiki Meya kiliundwa kwa fito za mti gani?

Alama ya hisi (!)
Alama ya hisi hutumiwa:
(a) Katika vihisishi kuonyesha hisia tofauti. Mfano:
Mshangao – Salaale!
Mshtuko-Ala!
Masikitiko, huruma au majuto – Pole!
Furaha – Oyee!
(b) Kuigiza tanakali za sauti. Mifano:
1. Omondi ameanguka chini pu!
2. Ng’ombe amezama majini zi!
Kistari kirefu (-)
Kiakifishi hiki hutumika:
(a) Kutoa maelezo zaidi kuhusu jambo.
Mifano:
1. Sera- uliyetaka kuzungumza naye, ameondoka.
(b) Kutoa orodha ya vitu.
Mfano:
Darasa letu lina:
– chaki
– kifutio
-Dawati

Kistari kifupi (-)
(a) Hutumika kuonyesha mzizi wa neno.
  Mifano: -baya,  -zuri, -angu, – chafu
(b) Kutenganisha tarakimu katika
tarehe.
Mfano: 6-7-2020, 18-08-2020
(c) Kuonyesha muda fulani wa kufanyika kwa jambo.
Mfano:
1. Saa 4:30-11:00 asubuhi (saa kumi na nusu hadi saa tano kamili)
2. Jumatatu-ljumaa (Jumatatu hadi ijumaa)
(d) Kuunganisha maneno mawili tofauti na kuunda neno moja.
Mfano: Mwana-haramu, Isimu-Jamii,
Semi-koloni
(e) Kuendeleza neno ambalo halijakamilika katika msitari ufuatao.
Mfano. Dadake Khadija alionywa na mjombake dhidi ya kute-
mbea barabarani usiku.
Semi-koloni (;)
Semi koloni pia huitwa nusu koloni au nukta mkato.
 Alama hii ya uakifishaji hutumika kuunganisha kwa kuelezea mawazo makuu katika sentensi.
Mfano:
1. Ukisikia amepiga unyende; huenda amenyang’anywa mkoba wake.
2. Wanapendana sana;wiki ijayo watafunga ndoa.
Nukta mbili (:)
Nukta mbili pia huitwa koloni. Alama hii hutumika:
(a) Katika kuorodhesha vitu mbalimbali.
Mfano:
1. Ukienda dukani niletee: kitabu, kalamu, wino, kifutio na kichongeo.
2. Yafuatayo ni majina ya wadudu:Tekenya,Nyungunyungu,Nondo.
(c) Kuonyesha saa. Mfano:
1. Mahujaji walifika saa 3:15. (Saa tisa na robo)
2. Vipindi shuleni mwetu huanza saa 7:45. (Saa mbili kasorobo)
(d) Katika mazungumzo kutenganisha jina la mnenaji na aliyoyanena.
Mfano
Daktari: Eleza unavyohisi.
Selemani: Ninahisi joto jingi mwilin
Daktari: Umetumia dawa yoyote?
Selemani: Ndio. Nimemeza tembe.
(e) Kuonyesha mada katika barua rasmi. Mfano;
KUH: NIDHAMU SHULENI
(f) Katika kumbukumbu za mkutano.
Mfano: Kumb 1/2015: Ununuzi wa vitabu.
Mabano au parandesi () {}
Matumizi ya mabano ni:
(a) Kutoa maelezo zaidi. Mifano:
1. Paka wangu (niliyepewa juzi) ndiye mshindi.
2. Njia hii (inayokarabatiwa) ikitumiwa itarahisisha uchukuzi.
3. Maji haya (niliyoyanunua) yana madini muhimu.

(b) Kutolea maelezo zaidi kuhusu neno au sentensi, Mifano:
1. Mfanyakazi aliyepokea kadhongo (hongo) alikamatwa na polisi.
2. Shangazi yangu (Bi Zuhura) ana rinda zuri.
3. Msimu wenye baridi nyingi (kipupwe) huogopwa na watu wengi.
Mkwaju / au
Alama ya mkwaju pia huitwa alama ya mkato, mshazari au mlazo. Alama hii hutumika:

(a) Badala ya maneno ‘au’ na ‘ama’.
Mfano:
1. “Tafadhali mtume Moraa/Mong’ina”, mwalimu aliniambia.
2. Kijiko/uma hutumiwa kulia chakula.
(b) Kuonyesha kisawe cha neno.
Mifano: Ugali/sima, gari/motokaa runinga/televisheni
(c) Katika uandishi wa tarehe ili kutenganisha tarehe, mwezi na mwaka. Mifano:
Tarehe 2/10/2020,Tarehe 1/1/2021
Alama za dukuduku (..)
Alama za dukuduku hutumika:
(a) Kuonyesha maneno yanayotangulia hayajaandikwa. Mfano:
1. .akawatuma uwanjani.
2. ..nikajua kuwa ukupigao ndio ukufunzao.
(b) Kuonyehsa usemi usiokamilika.
1. Kaisha alipokuja kwetu.
2 Asiyesikia la mkuu…
3. Lisemwalo…
Vinukuu (” “)
Vinukuu pia huitwa vinukuzi au alama za mtajo. Hutumika katika kunukuu usemi 
halisi. Mfano:
1. “Uje ofisini kesho, meneja alimwambia mfanyakazi.
2.Ni nani atakayetoa ushahidi mahakamani? Wakili alimuuliza mshtakiwa.
Alama ya king’ong’o (‘)
Alama ya king’ong’o pia huitwa ritifaa
Huonyesha maendelezo ya sauti ya Ung’ ong’o
Mfano :
ng’ang’ana, ng’ombe, ng’oa.
ng’amua

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *