KURUNZI YA LUGHA

12.Nilitamani- Phibbian Muthama. Mtiririko

Nilitamani- Phibbian Muthama. Mtiririko Tumaini(Msimulizi) yuko katika hali ya kutanga huku njaa imemzidi, kwani hajala tangu jana ila chai rangi aliyokunywa usiku, ila ana matumaini ya maisha bora. Ameondoka kwa Nina awali, anayemkaribisha katika nchi hii ya Wabongo na kuishi naye kama mwanawe kwa muda. Tumaini alimwacha mwanawe wa pekee na bibi yake, Farida. Nina …

12.Nilitamani- Phibbian Muthama. Mtiririko Read More »

11.Nipe Nafasi- Mzamane Nhlapo Mtiririko

Nipe Nafasi- Mzamane Nhlapo Mtiririko Mamake msimulizi anaamka huku macho yamesharabu wekundu. Baba yao hawatumii pesa kutoka Afrika Kusini anakofanya kazi migodini. Mama anaamua waende Makongeni kwa jamaa ya baba badala ya kuwatazama wanawe wafe njaa. Wanaabiri basi kutoka Habelo, kijiji wanachoishi, mjini Mbote. Wanafikia mwisho wa barabara na kushuka basi. Wanaipanda Milima ya Maloti …

11.Nipe Nafasi- Mzamane Nhlapo Mtiririko Read More »

10.Toba ya Kalia- Douglas Ogutu. Mtiririko

Toba ya Kalia- Douglas Ogutu. Mtiririko Jack anapokea simu ya Kalia, babake Siri, rafikiye mkubwa tangu utotoni. Ujumbe ni kuwa Siri atakuwa hewani kwenye runinga ya Kikwetu, na ameagiza Jack na wazazi wake (Siri) wawepo. Anavaa shati alilolainisha kwa kuweka chini ya godoro na suruali ya khaki. Hali hii ni kwa kuwa anawekeza kujiendeleza kimasomo. …

10.Toba ya Kalia- Douglas Ogutu. Mtiririko Read More »

9.Ahadi ni Deni- Rayya Timammy Mtiririko

9.Ahadi ni Deni- Rayya Timammy Mtiririko Fadhumo anajiunga na shule nzuri ya upili. Anapelekwa na babake mjini na kumnunulia kila anachohitaji. Wanaagana baada ya Fadhumo kumsisitizia atatia bidii na kufaulu. Babake anamuaga akisema anarudi kwa raha akijua atatia bidii kwa ajili yake mwenyewe na familia. Yanaondokea kuwa maneno ya mwisho ya babake. Wanapanga akae kwa …

9.Ahadi ni Deni- Rayya Timammy Mtiririko Read More »

8.Kifo cha Suluhu- Dominic Maina Oigo. Mtiririko

8.Kifo cha Suluhu- Dominic Maina Oigo. Mtiririko Abigael na Natasha wanasimuliana masaibu yao yanayowalazimu kuwa kupe wa kunyonya wanaume. Wamekulia eneo moja na kupatana na hali ngumu ya maisha hadi wakakinai. Abigael yuko mwaka wa tatu na kapitia taabu tele. Ameomba na kutafuta misaada, hata kwa gavana lakini hapati. Natasha naye amesoma kwa zaidi ya …

8.Kifo cha Suluhu- Dominic Maina Oigo. Mtiririko Read More »

7.Kila Mchezea Wembe- Pauline Kea Kyovi Mtiririko

7.Kila Mchezea Wembe- Pauline Kea Kyovi Mtiririko Hadithi ni barua kutoka Hospitali ya Uhai ni Neema inayoandikiwa Emmi na mpenziwe, Tembo. Nia kuu ni kuomba msamaha huku akimweleza mwenziwe yaliyomsibu, akikiri makosa yake. Bado yuko kitandani, japo ameimarika kidogo. Anaweza kusema kwa kulazimisha na chakula kinapita kooni, ila hajadiriki kuona. Maisha humo ni mazito upande …

7.Kila Mchezea Wembe- Pauline Kea Kyovi Mtiririko Read More »

6.Mzimu wa Kipwerere!- Yussuf Shoka Hamad Mtiririko

6.Mzimu wa Kipwerere!- Yussuf Shoka Hamad Mtiririko Mzimu wa Kipwerere unatisha sana. Mzimu wenyewe ni wa kichaka kidogo kilichojaa aina tofauti ya miti iliyobanana na kusabababisha kiza kinene cha kutisha. Kitisho cha kwanza ni kichaka hicho kuitwa mzimu. Pili, kichaka hicho kiko kwenye kiwanja kipana kilichozungukwa na nyumba za wanakijiji. Jina Kipwerere linatokana na jamaa …

6.Mzimu wa Kipwerere!- Yussuf Shoka Hamad Mtiririko Read More »

5.Sabina- Winnie Nyaruri Ogenche Mtiririko

5.Sabina- Winnie Nyaruri Ogenche Mtiririko Ni Jumapili ya mwisho kabla ya mtihani wa kitaifa kuanza. Sabina anawazia mtihani pamoja na ufadhili wa shule ya bweni unaomsubiri iwapo atafaulu. Hata hivyo, anashangaa itakuwaje akifeli. Anakumbuka maneno ya mwalimu kuwa mizizi ya elimu ni michungu ila matunda ni matamu. Anagutushwa na wito wa Yunuke, na hapo anainuka …

5.Sabina- Winnie Nyaruri Ogenche Mtiririko Read More »

4.Harubu ya Maisha- Paul Nganga Mutua Mtiririko

4.Harubu ya Maisha- Paul Nganga Mutua Mtiririko Utulivu wa mazingira unamsahaulisha msimulizi(Kikwai)  mpito wa wakati hadi anapopokea simu ya Mama Mercy(mkewe) akilalamika kuwa mtoto atalala. Anagundua ni saa nne kasorobo usiku na kufunga kazi na kuondoka ofisini.Hakuna msongamano wa magari. Anapofika Kenyatta Avenue, anagundua simu inaita. Ni mamake amepiga. Haipokei bali anaamua kumpigia akifika nyumbani. …

4.Harubu ya Maisha- Paul Nganga Mutua Mtiririko Read More »

3.Mapambazuko ya Machweo- Clara Momanyi Mtiririko.

3.Mapambazuko ya Machweo- Clara Momanyi Mtiririko. Mzee Makucha na Mzee Makutwa ni marafiki, ambao wamestaafu na umri wao umesonga. Hata hivyo, urafiki wao uliokolea awali sasa umepungua, umebaki tu ule wa kujuliana hali. Mzee Makutwa anaonekana akizurura mtaani na gari lake baada ya kustaafu, wala hakuna ajuaye shughuli zake, hata Mzee Makucha. Anaonekana tu kila …

3.Mapambazuko ya Machweo- Clara Momanyi Mtiririko. Read More »

2.Msiba wa Kujitakia- D. W. Lutomia Mtiririko wa hadithi

2.Msiba wa Kujitakia- D. W. Lutomia Mtiririko wa hadithi Wakazi wa Matopeni wako katika kipindi kigumu sana cha maisha, taabu zinawaandama kila uchao wala hawana wa kumlilia. Machoka ni mmoja kati ya Wasakatonge wanaoishi mtaa wa matopeni. Amefika nyumbani jioni akitoka katika shughuli za kutafuta kibarua ili kupata cha kutia tumboni lakini hajaambulia chochote. Anaona …

2.Msiba wa Kujitakia- D. W. Lutomia Mtiririko wa hadithi Read More »

1.Fadhila za Punda- Rachel Wangari. Mtiririko

1.Fadhila za Punda- Rachel Wangari. Mtiririko Lilia anagutuka kutoka usingizini kwa hofu. Anamsubiri mumewe Luka. Amelala kochini ili amfungulie haraka. Anagundua kwamba bado hajafika kama alivyodhania, lakini hili halimpunguzii hofu, kwani ana hakika kuwa atakuja tu, tena kwa hasira tele kwa kukosa kupokea simu yake, ambayo ilipigwa akiwa bafuni. Ni saa nane za usiku na …

1.Fadhila za Punda- Rachel Wangari. Mtiririko Read More »

MWONGOZO WA MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE

Utangulizi Mwongozo huu una nia ya kuwa mwanga gizani kwa wasomi wa diwani ya ‘Mapambazuko ya Machweo na Hadithi nyingine, kwa kutoa maelezo maridhawa kuhusiana na hadithi tofauti zilizomo humu. Ili kufanikisha hili, mwongozo huu umeangazia masuala kadhaa katika hadithi. Kabla ya kwenda katika hadithi binafsi, ni vyema kuangazia vipengele Fulani vya diwani. Mada: Mapambazuko …

MWONGOZO WA MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE Read More »

WIMBO WA NGAZI

Wimbo wa ngazi Kila jinsia na rika  Makabila ya watu Tulizunguka kijijini Kwa lengo na sauti moja Nyuso zilitumwekamweka kwa furaha  Wanyonge tulichangamka na kukaramka Vipofu Viziwi  Na viwete  Tukakusanyika kwa pamoja kama nyuki Ili tuifanikishe siku yako  Ajabu!  Asubuhi saa kumi ukiwa unakorota  Tayari tulikuwa foleni  Watoto wachanga wakitulilia migongoni  Tukakukabidhi ngazi kwa furaha …

WIMBO WA NGAZI Read More »

NGANO

Ngano ni ule utungo, hubuniwa kufundisha Huelezwa kwa mpango, uweze kuburudisha Uwe kweli na urongo, jamii hufunganisha Mtambaji ni fanani, mwenye lugha  natharia Ainaze ni hekaya, mazimwi yakishetani Khurafa wanoongeya, na mashujaa fulani Kuna za mafumbo piya, zenye maana ya ndani Visasili mitanziko,mwisho wake ni usuli. Wahusika wa hekaya,wakuu ni binadamu. Wabunifu nakwambiya,wajanja walohitimu Wachekesha …

NGANO Read More »

VITATE

VITATE Vitate ni maneno yanayotatanisha kwa sababu ya ukaribu uliopo kimatamshi na kimaendelezo baina yake. Mifano ya vitate: Wasiwasi-jakamoyo, wahaka au shaka. Waziwazi-bila ya kuficha. Dhamini-wekea mtu ahadi kuwa utatimiza jambo fulani. Thamini-tia maanani au heshimu.K.m Asiyekujua hakuthamini. Bamba-lazimisha mtu kufanya ngono naye. Pamba -chakula cha wakati wa safari.             …

VITATE Read More »

Uakifishaji

Uakifishaji Neno uakifishaji linatokana na kitenzi ‘akifisha’ chenye maana ya kutumia alama za lugha ifaavyo katika maandishi. Sarufi ya lugha yoyote ile hutegemea uakifishaji ufaao. Kikomo (.)  Kikomo pia huitwa nukta, kituo au kitone. Matumizi yake ni : (a) Kuonyesha mwisho wa sentensi. Mifano: 1. Kababy ameenda ughaibuni. (b) Katika uandishi wa tarehe ili kutenga …

Uakifishaji Read More »

TAHAKIKI YA UMBILE

Mwanamke Alikuwa mwanamke wa elfu. Hakika, Mungu alikuwa amempoteza hurulaini wake peponi. Meno ya bisi/mchele yaliyopangwa yakapangika kinywani kama lulu katika chaza/bao katika vidu/kete. Mwanya wa haiba na mvuto /mwanya wa mwangaji. Midomo ya miteko na kasiba. Vidu vilivyoshobweka barabara mashavuni. Urembo wa sahani. Macho ya chawa kama Mchina au Maninga ya gololi/kikombe Pua ya …

TAHAKIKI YA UMBILE Read More »

Msamiati wa wafanyakazi

Msamiati wa wafanyakazi  Kazi ni shughuli yoyote halali afanyayo mtu ili kukimu mahitaji yake.Watu hupata kazi hizo kutokana na masomo yao au tajriba na uzoefu. Mifano ya wafanyakazi: Tabibu – Mtu aliye na utaalamu wa kuwatibu wagonjwa. Dereva – Mtu anayeendesha gari. Bawabu – Mtu anayelinda lango. Muuguzi au nesi– Mtu anayemsaidia daktari kuwapa wagonjwa dawa na kuwatunza. Tarishi au katikiro– Mtu anayefanya kazi …

Msamiati wa wafanyakazi Read More »

VIBADALA

VIBADALA Kibadala ni neno linalotofautiana kidogo na neno jingine kimatamshi lakini lenye maana sawa. Mifano ya vibadala  Alfeni -elfeni  Alfu -elfu Arusi -harusi Angalao -angalau Afisa -ofisa Blanketi -blangeti Barobaro -barubaru, Banki -benki Bakara-bakari Bufeti -bufee Chakuleti-chokoleti Darahimu -dirhamu Desturi -dasturi Disemba -Desemba Ekari-Eka Faraji-faraja Firauni-farao Fikra-fikira Guruneti-gruneti Gulamu-ghulamu Gagulo-gagro Haleluya-aleluya Jumuiya-jumuia Jagina-chagina Kabeji-kabichi Kibiongo-kibyongo Kichinjamimba -kitindamimba …

VIBADALA Read More »

METHALI HALISIA

METHALI HALISIA Hizi ni methali zinazomwelekeza mtu kuhusu hali fulani ya kimaisha. Maisha ni ahadi, itimize Maisha ni fursa, itumie. Maisha ni zawadi, ipokee. Maisha ni tatizo, litatue. Maisha ni jasiri, jasurika. Maisha ni ubishi, yakabili. Maisha ni kiwambo, yatazame. Maisha ni bahari, yaogelee. Maisha ni mazoea, yazoee. Maisha ni stara, staarabika Maisha ni fumbo, …

METHALI HALISIA Read More »

ULEMAVU

ULEMAVU Kilema/Uatilifu –ni kasoro iliyoko kwenye kiungo au viungo vya mwili. Mlemavu – ni mtu au mnyama mwenye kasoro ya kiungo au viungo. A)Hali ya ulemavu Mafungamavi -Miguu iliyopindika kwa ndani. Kidazi -Ukosefu wa nywele kichwani.Pia upara. Kigutu -Kiungo cha mwili kilichokatika. Upara-Hali ya kutokuwa na nywele kichwani. Mangombo -Miguu iliyobinukia mbele. Matege -Miguu iliyopindika kwa nje na kuacha nafasi kati …

ULEMAVU Read More »

NAOGOPA.

NAOGOPA. Uko wapi mama Boi,kunyesha bado kungali Nonavyo sitoboi,niletee muwavuli Wandamane na kikoi,baridi shadidi kali Ikiwa mwanga umekosa,nawe tumia akili. Niendapo sitafika,nimeola giza kuu Mvua inamwaika,yatateleza maguu Chinile nitaanguka,ninuwe miguu yuu Njoo hapa mwanga wangu,’tumiye hino akili Muhibu fanya haraka,natapia kwenda too Tumboni naangaika,naomba haraka ndoo Mapema usipofika,hapa nitashika moo Kwa kutii fanya hara,matumbo yakorogana.

VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE

 VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE  A  Adui lakini po pote uendako yuko nawe-Inzi Afahamu kuchora lakini hajui achoracho- Konokono Aliwa, yuala; ala, aliwa-Papa Ajenga ingawa hana mikono- Ndege Ajifungua na kujifunika-Mwavuli Akitokea watu wote humwona-Jua Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni-Ugonjwa Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza- Mgomba Alipita mtu ana bunda …

VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE Read More »

Ushairi

Ushairi Shairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na Mpangilio maalumu wa maneno ili ujumbe unaokusudiwa uwasilishwe. Sifa za Ushairi Shairi huwa na umbo mahsusi Hutumia lugha ya mkato Huwa na beti,Mizani,Mishororo na vina Hukiuka kanuni za kisarufi Hutumia lugha teule yenye kuibua hisia nzito Hutumia tamathali mbalimbali za usemi Istilahi za kishairi Hizi …

Ushairi Read More »

ISIMU JAMII

ISIMU JAMII Isimujamii – Ni taaluma inayochunguza uhusianouliopo baina ya lugha na jamii. Hasa hushughulikia jinsi watu wanavyotumia lugha katika jamii. Isimu- ni uchunguzi wa lugha kisayansi. Jamii – ni kundi filani la watu wenye uhusiano fulani. Mambo yanayoshughulikiwa katika isimu jamii i)   Tofauti katika lahaja za lugha kama vile Kiswahili cha lamu(kiamu), cha Mombasa(kimvita), cha unguja(kiunguja), cha bara. ii)  Tofauti katika matumizi ya lugha baina ya makundi tofauti tofauti katika jamii. Mfano wazee na watoto,vijana na wabunge. iii) Matumizi ya lugha kutegemea miktadha tofauti kama vile kazini, nyumbani, sokoni, n.k. iv) Mtazamo wa watu kuhusu lugha. Je, wanaitukuza au wanaitweza? v)  Jinsi mtu anavyotumia lugha kutegemea uhusiano na wazungumzaji au mada husika. vi) Lahaja mbalimbali za lugha ya Kiswahili. Umuhimu wa isimu jamii. i)   Huwafunza watu kaida za lugha ili waweze kuitumia ipasavyo kutegemea mila na desturi. ii)  Humsaidia mzungumzaji au mwandishi kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha na usahihi. iii) Humpa anayetumia lugha uwezo wa kutambua, kutofautisha na kutumia mitindo mbalimbali ya lugha kutegemea mahitaji. iv) Hufunza maadili ya jamii hasa yanayohusiana na matumizi ya lugha kutegemea uhusiano. Mf. Mtu na mkwewe, mtoto na mzazi, mwajiri na mwajiriwa. v)  Hufunza mbinu za mawasiliano pamoja na mbinu za kupata maana kamili. vi) Hudhihirisha utamaduni wa jamii. vii) Humsaidia msemaji au mwandishi kutambua makosa mbalimbali yanayojitokeza wakati wa kuzungumza au kuandika. viii)  Hufunza mbinu za kuwaelewa watu tunaotagusana nao kwa kuzingatia mambo k.v hadhi, utamaduni hivyo utangamano. Maana ya mawasiliano. Utaratibu ambao huwawezesha viumbe kupashana ujumbe ambao unahusisha mwasilishi na mpokeaji wa ujumbe. Njia ambazo kwazo mwanadamu huwasiliana. i)    Mgusano na ukaribianaji ii)  Mavazi iii) Sauti iv) Ishara za mwili. Lugha Ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa na wanadamu katika mawasiliano. Sifa za lugha. i)   Hakuna lugha iliyo bora kushinda zingine. –zote ni sawa. ii)  Kila lugha ina sifa zake. iii) Lugha hubadilika kutegemea mazingira, aina ya tukio, wakati na matumizi ya lugha hiyo. iv) Lugha ina uwezo kukua, mfano Kiswahili kimebuni msamiati TEHAMA (Teknolojia ya habari na mawasiliano.) v)  Lugha pia hufa kwa msamiati wake kupotea n.k …

ISIMU JAMII Read More »

INSHA

INSHA Utungo unaoundwa kwa mfululizo wa sentensi zinazozungumzia jambo, tukio au kitu fulani Aina 1.   INSHA ZA KAWAIDA a)   Insha ya Picha  Ambapo mwanafunzi amepewa picha kadha na kutakiwa kutunga kisa na kueleza yote yanayotokea kwenye picha hizo. Chunguza vizuri ujue kinachotokea katika hizo picha. ü  Kichwa kiafikiane na picha ulizopewa. Kila picha ipangwe na kuwa na aya …

INSHA Read More »

TANAKALI ZA SAUTI

            Moyo kupapa papapa ·       Jaza pukupuku ·       Timka timtim – nywele zilimtimka  timtim ·       Chanika chanechane ·       Koma komekome ·       Chanua chanuchanu ·       Mambo kuvurugika vuruguvurugu ·       Tokwa na jasho jekejeke ·       Fafanua  kinaganaga/kinagaubaga/kimasomaso ·       Gugumiza gugugu ·       Batana batabata ·       Moyo kudunda dududu ·       Maskini hohehahe/hahehohe/kupindukia ·       Tafuna tafutafu ·       Tetwereka tepweretepwere ·       Kamata patupatu ·       Penya fya ·       Saga tikitiki ·       Bung’aa ng’aa ·       Miminika bwaibwai ·       Zama zii ·       Saa …

TANAKALI ZA SAUTI Read More »

Masharti ya kisasa

MUHTASARI Kisa hiki kinahusu Kidawa, mwanamke mrembo ambaye alipendwa na muuza samaki aitwaye  Dadi. Dadi alimpenda sana Kidawa na akataka amchumbie awe mkewe. Kidawa alimkataa Dadi na kumkwepa kabisa. Hata hivyo, mambo yalibadilika ambayo yalimshangaza sana Dadi. Kidawa  alimwambia kwamba yu radhi  kuolewa  na  Dadi kwa  masharti ya ndoa  ya kisasa. Dadi kwa  shangwe alizonazo …

Masharti ya kisasa Read More »

KILIMO

                                       Kilimo ni kazi ya kulima na kupanda mazao shambani.  Pia huitwa zaraa. ifuatayo ni mifano ya misamiati ya kilimo. Shamba– ardhi iliyolimwa na kupandwa mazao.  Pia konde. Weu-kipande cha ardhi kilicholimwa na kutayarishwa ili kupanda mbegu au miche.Pia …

KILIMO Read More »

MAAMKIZI

Maamkizi / maamkio / utweshi Maamkizi hutumika kujuliana hali. Ni maneno ya kuamkiana. Kuna maamkizi yanayoweza kutumika nyakati zozote na baina ya watu wowote. Maamkizi na Majibu 1. Habari? – njema/nzuri 2. Uhali gani? – njema/nzuri 3. Je la utu? – sina utu 4. Waambaje? – sina la kuamba/salama 5. Sabalkheri? – sabalkheri/aheri 6. Masalkheri? …

MAAMKIZI Read More »